Ruby amlilia Ali Kiba, adai amemfananisha na Mbwa





Wikendi iliyopita ilikuwa ndefu kwa mwimbaji Ruby ambaye alijikuta akikwazika na kumtuhumu Ali Kiba kwa kumfananisha na mbwa wake na kuamua kuweka kilio chake mtandaoni, hali iliyopelekea mashabiki wa mwimbaji huyo wa ‘Mwana’ kuzidi kumharibia wikendi yake kwa mashambulizi ya matusi.
Ruby alimsikiliza Ali Kiba akieleza kwenye kipindi cha The Sporah na kudai kuwa amempa mbwa wake jina la mwimbaji huyo wa kike. Kufuatia kauli hiyo Ruby alianza kutiririsha maelezo kwenye mtandao.
“Well well well
Kabla ya yote naombeni sana mashabiki zangu, mniwie radhi kwa nnacho kiandikia katika ujumbe huu binafsi mimi sijapendezewa kabisa na alichokisema kaka yangu @officialalikiba kwenye kipindi cha @thesporahshow kilichorushwa kupitia @cloudstv kaka yangu alikiba mimi ni mdogo sana kwako si kwa umri wa kimuziki, sikutegemea na sijapendezwa na kauli yako yakunifananisha mimi na MBWA mimi ni binaadam na ni mdogo wako kama alivyo @zabibu92kiba sidhani kama ungeweza kumwita huyo mbwa wako zabibu au abdul, mimi sina ukaribu wowote na wewe lakini kama mtu niliyemkuta kwenye industry na uliyenitangulia kuliona jua na mpaka uliponifwata kuniambia una- appreciate kazi yangu nakuniomba nifanye nyimbo na mdogo wako @officialbdukiba na nikakubali yote hayo yalifanikiwa kutokana na love niliyokuwa nayo kwako kama kaka yangu,hujawahi hata siku moja kunitamkia kwamba unambwa wako anaitwa Ruby, kwa sababu mimi na wewe tumesha kutana nakuongea si chini ya mara moja, hujawahi kusema hilo kwangu, ila umekuwa ukiniambia tu naimba vizurii, je ulisahau nini kaka yangu hadi kushindwa kuniambia muhusika wa jina la mbwa wako mpya,mimi nimeona ni kejeli na dharau kubwa na hazisaidii katika maisha zaidi ni kujishushia heshima yako haipendezi kwa mtu kama wewe ambae pia unaangaliwa na watu wengi kama kioo cha jamii,nategemea kuona mfano mzuri kutoka kwako nikiwa kama mdogo wako lakini umenitia giza machoni @officialalikiba kakaangu kwakweli nimekwazika sana kwasababu mimi ndo kwanza naanza game naanza kazi ya kuendeleza nchi hii na afrika kwa dunia nzima kwenye upande wasanaa ambao wewe umeshaanza muda ,lakini nimestaajabu unanifananisha na mbwa ,cha ajabu zaidi hata watu wako wa karibu @rehemavisuallab @zabibu92kiba hawaitamki wala kuileta katika jamii kwa usahihi wa mbwa kweli ,Naamini Mungu hamtupi mja wake, chozi la mnyonge haliendi bure, Me namuachia Mungu”
Baada ya maelezo hayo, Ali Kiba aliamua kubofya batani za simu yake kutoa ufafanuzi kwa kile alichokisema. Kiba Sakata hilo liliwafikia wakuu baada ya Ali Kiba kuupigia simu uongozi wa Ruby na kuomba radhi. Ruby alirudi kueleza kilichotokea na huenda sasa mambo yako sawa kati yao.  “Asante sana kaka @officialalikiba Msamaha wako nimeupokea na nimekubali japo umeondoa post yako. Utakuwa na sababu zako unazojua mwenyewe. Kama nilivyosema mwanzo issue sio jina la mbwa wako, issue ni huo ‘mfugo’ uliofanywa topic na watu wako wa karibu na kunifanya nianze kuhisi huenda ulikuwa na maana nyingine. Since umepiga simu kwa boss wangu kuomba radhi, mimi sina kinyongo, naomba Mungu huyo mbwa awe anabweka tu ha ha,tufanye tu kazi kaka.”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA