Aibu! Vunja Jungu yamtokea Puani Njemba…Anaswa akila URODA na Mke wa Mpangaji wake GESTI
Vunja jungu! Saa kadhaa kabla ya kuanza kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali ameibua sekeseke kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti), kisa kikidaiwa ni mchepuko akihusishwa na mke wa mpangaji wake, Ijumaa Wikienda lina kisa na mkasa. Wakati ikirandaranda mitaani kutega mingo, Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea mchongo kuwa kuna timbwili kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar ambapo walifika eneo la tukio na kushuhudia kasheshe hilo la aina yake. OFM ilimshuhudia mzee huyo akichomolewa kutoka chumbani huku damu zikimvuja baada ya kula kichapo kutoka kwa jamaa na ndugu wa mwanaume aliyedai kuwa jamaa huyo alikuwa anamsumbua mkewe. Jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Lugali akihusishwa kuchepuka na mke wa mpangaji wake, akiwa amenaswa kwenye gesti moja maeneo ya Buguruni, Dar. Kwa mujibu wa mashuhuda, kabla ya jamaa hao kuingia chumbani humo kwanza walivunja mlango wa chumba hicho baada ya kupata ...