JESHI LA POLISI LAOMBA MSAADA KUTOKA JESHI LA JWTZ KUSAIDIA VITA DHIDI YA MAJAMBAZI
Siku moja baada ya majambazi kuvamia Benki ya Access Tawi la Mbagala Rangi Tatu, kuua watu watatu akiwamo Polisi na kujeruhi watu wengine watatu akiwamo polisi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amesema wataomba msaada wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ili kukabiliana na matukio ya ujambazi. Alisema Jeshi la Polisi linajipanga upya kuhakikisha wananchi wanakuwa na amani kwa kuwashughulikia majambazi popote walipo. Waziri Kitwanga alisema wanaanza na Mkoa wa Pwani, kwa kuhakikisha wanawasaka na kufyeka mapori yote ya Bagamoyo na kwingineko ili kuvunja mtandao wao. “Kama walidhani Jeshi la Polisi limelala lipo macho, walichofanya ni kama wamemuamsha aliyelala, tutawasaka, tutawakamata na tutawapeleka kwenye mkono wa sheria na tutahakikisha tunawamaliza wote,” alisema Kitwanga. Alisisitiza kuwa wanaotumia pikipiki nguvu ya ukaguzi itaongezwa dhidi ya vyombo hivyo, kwa sababu inaonekana wahalifu wengi hasa majambazi hutumia usafiri huo kutekeleza ...