WEMA ATOSWA VIKAO VYA HARUSI YA DIAMOND
Meninah
habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah
ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa
mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe
na Queen Darling ambaye ni dada wa Diamond.
Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine paparazzi wake alienda nyumbani kwa
Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta
Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia
upande wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema
bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza
kwa mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah
walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo
za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia
mapenzini kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja
lilipovujisha habari hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media
nyinmgine kuziandika kwa kasi
Maoni
Chapisha Maoni