Mwanzilishi wa kampuni ya 'Apple' aliwazuia watoto wake kutumia iPad, iPhone na iPod, fahamu sababu;
Tumesikia watu wakiachana ama familia zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya Apple. Mwaka jana familia moja nchini China iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua iPhone5.
Kwa kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple na mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi zaidi bidhaa hizo.
Na huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao zingeweza kuwa za mfumo wa simu za kisasa za kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya hali ya juu ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo huo.
Lakini ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs hakuwaruhusu hata kidogo watoto wake kutumia iPhones, iPods wala iPads nyumbani kwake.
Katika article iliyoandikwa na New York Times wiki hii, mwandishi wa habari Nick Bilton ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya Steve Jobs alipomuuliza jinsi ambavyo watoto wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.
“Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia nyumbani.” Alijibu Steve Jobs.
Nae mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter Isaacson ambaye alikuwa akitumia muda mwingi nyumbani kwa boss wake huyo alithibitisha kuwa maoengezi ya uso kwa uso yalitawala katika nyumba hiyo.
“Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha usiku na familia yake kwenye meza kubwa jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au computer. Watoto hawakuonekana kuwa addicted hata kidogo na vifaa hivyo.” Alieleza Isaacson.
Inaelezwa kuwa hata Steve Jobs hakuwa na tabia ya kutumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Steve Jobs aliyefariki mwaka 2011 sio mtu maarufu pekee aliyeamini katika kuweka sheria kali kwa watoto wake kutumia vifaa hivyo, Chris Anderson, mhariri wa zamani wa Wired pia alieleza kuwa yeye na mkewe wamewazuia watoto wao kiasi kwamba watoto hao huwalalamikia sana wakilinganisha na uhuru wanaouona katika familia za mafiki zao.
Utafiti uliofanywa katika eneo la Chuo Kikuu cha California, Los Angeles na kuchapishwa hivi karibuni unaonesha kuwa siku chache baada ya kuzuia watoto kutumia vifaa vya kieletroniki vya simu, ufaulu wa watoto katika masomo ulipanda ghafla.
Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani watoto nchini Marekani hutumia zaidi ya saa saba na nusu kwa siku katika matumizi ya simu za kupangusa na vifaa vingine vya kielekroniki kama iPads, iPod n.k.
Uamuzi ni wako, kumnunulia mwanao vifaa vya hivyo au kumuweka mbali na mapinduzi hayo ya kiteknolojia.
Maoni
Chapisha Maoni