Martin Kadinda: Wema Sepetu Hana Pesa Ya Kunilipa

Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwasasa hana pesa ya kumlipa bali yeye Martin anahangaika kwa issue zake binafsi ili wasilale njaa…

Kadina amesema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo kishkaji zaidi.
 
“Wema hana pesa ya kunilipa mimi, ninachokifanya ni  kuhangaika kutafuta deals ili mimi na yeye  maishani tusilale njaa, maisha ni kutegemeana.
 
“Kikubwa ninachofanya ni kutafuta dili za kazi nyingi ili tuweze kupeana pasu kwa pasu lakini si mshahara, nafanya kazi na bosi wangu Wema kishikaji na kwa kweli nafurahia sana utaratibu huu”
 
Martin alisema kuwa kama angekuwa na mkataba na Wema kumlipa kila mwezi asingemudu na kusema yupo na Wema kwasababu anajua ni mtu wa aina gani na anafanya kazi zake kwa uhuru bila kubanwa.
Martin Kadinda akiwa na Wema Sepetu.
Martin Kadinda akiwa na Wema Sepetu.
 
Wakati Wema yupo kimapenzi na yule kigogo aliyejulikana kwa jina la Clement(CK),  Wema alidaiwa kumwaga pesa kila kona na wapambe kibao wa kula bata nao huku akiwa na magari kadhaa lakini kwasasa anadaiwa kushuka kiuchumi na kubaki na gari moja pekee huku wapambe aliokuwa nao wakitimua na waliobaki kulalamika hawali bata kama zamani.

Hivi karibuni tena Diamond Platnumz aliye mpenzi wa Wema alisema kuwa Wema ni mtu wa starehe na kuendekeza mashoga wapenda anasa badala ya kutumia fursa na umaarufu mkubwa alionao sasa kufanya kazi zake kwa bidii hususani filamu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA