TAARIFA KAMILI MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO CHA POLISI WAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA,KUUA ASKARI 2,KUIBA SILAHA
Majambazi
wameingia na kuvamia kituo cha polisi Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita
kisha kuua askari wawili, kujeruhi wengine wawili kisha kupora bunduki
kumi risasi na mabomu ya mkono kisha kutokomea pasipo kukamatwa.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo majambazi hao walivamia
katika kituo kikuu cha polisi Wilaya ya Bukombe Mkoani saa 9 alfajiri
wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurusha kwa mkono.
Mwandishi wa Malunde1 blog Victor Bariety anasema kwa mujibu wa
taarifa alizozipata ni kwamba majambazi hao walizingira kituo hicho hadi
eneo la mapokezi(CRO)na kuanza kuwamiminia risasi za moto askari
waliokuwa zamu.
Kufuatia hali hiyo askari wawili kati ya wanne waliokuwa kituoni hapo
walipoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za
miili yao.
Akiongea
na Malunde1 blog mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe Dkt Honorata
Rutatinisibwa amekiri kupokea miili ya askari wawili wa kike na
kiume ambao ni WP 7106 PC Uria Mwandiga na askari namba G.2615 Pc
Dustani Kimati.
Askari
waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwenye namba E.5831
CPL David Ngupama Mwalugelwa aliyejeruhiwa kichwani na usoni na kwamba
ameumizwa vibaya sehemu za midomo yake huku meno mawili yaking'oka na Mohamed Hassani Kilomo ambye amejeruhiwa kifuani na mguu wa kulia uliovunjika mfupa kwa kupigwa risasi.
Kwa mjibu wa Dr Honoratha kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya
wamewapa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa
tukio na kuahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Na Victor Bariety-Malunde1 blog-Geita
Maoni
Chapisha Maoni