Kiongozi wa Freemason aelezea alivyochumbia


KWA UFUPI
Mwandishi wa makala haya ni kiongozi mkuu mstaafu wa Freemason Afrika Mashariki, aliyetumikia taasisi hiyo kwa zaidi ya miaka 60.
 
Kifo cha baba yangu kiliniuma sana. Uhusiano wetu ulikuwa wa namna ambayo hata vijana wa siku hizi au jamii ya Lohana wasingeweza kuelewa. Upendo wangu kwa mama ulikiwa usio na masharti.
Kwa upande wa baba uhusiano tuliokuwa nao haukuwa na shaka. Tulikuwa tumeunganishwa zaidi ya mtu anavyoweza kudhani. Ulikuwa ni uhusiano ambao unazidi ule wa mtoto wa kwanza na baba yake katika jamii yetu.
Bahati mbaya uhusiano huo ulivunjika, hisia zangu za kumpoteza baba ziliathiri utambulisho wangu. Kama isingekuwa hivyo, ningekuwa na mke niliyempenda sana na mtoto wa kwanza. Kifo kile kiliacha pengo ambalo lilikuwa gumu kuliziba.
Kisha, kama ilivyotokea mke wangu mpenzi, Jayli alinionyesha upendo ulioweka mambo katika utaratibu uliokubalika. Hadi kufikia Agosti 1959 tulikuwa tayari tumeshakaa ndani ya ndoa kwa miaka minne. Mtoto wetu wa miaka mitatu, Manish alikuwa mjukuu wa kwanza wa kiume katika familia ya Chande.
Mtoto huyo alianza kuondoa uchungu wa dakika za mwisho aliokuwa ameniachia baba yangu. Uwepo wake nyumbani ulirahisisha mambo. Wakati huo nilikuwa siishi kwenye nyumba ya baba yangu Upanga. Tulikuwa tayari tumeshahamia kwenye nyumba yetu barabara ya Umoja wa Mataifa.
Kama ambavyo nimesema Jayli na mimi tulikuwa tunaishi kwa raha katika muda mfupi tu wa miaka minne tuliyokuwa tumeishi.
Hata hivyo, mawazo yangu kuhusu ndoa yalikuwa yakifikiria kuishi muda mrefu kuliko hapo. Miaka minane kabla kifo cha baba yangu na siyo muda mfupi kabla sijarudi Tanganyika kutoka India, mawazo ya kuoa yalianza kumwingia mjomba wangu Ratansi.
Ninasema mawazo yalianza kumwingia mjomba wangu Ratansi kwa sababu alikuwa mtu mzuri. Niliwapenda wasichana wakati huo, lakini moyo wangu haukuwa kwenye kuendeleza familia.
Hata hivyo, mjomba wangu, Ratansi aliyekuwa mtu wa taratibu, akiwa ndiyo kwanza ametoka kupona ugonjwa aliokuwa anaumwa, aligundua kuwa binamu yake nilikuwa nimefikia wakati wa kuwa na familia yangu.
Kwanza alianza kunisimulia habari za mimi kufunga ndoa walizokuwa wamezungumza na baba yangu mwaka 1951. Katika siku hizo mazungumzo kama hayo yalikuwa jambo la kawaida. Katika utamaduni wa Kihindi kaka wawili wanaweza kuzungumza mambo hayo na kupanga mikakati ya baadaye.
Pia huchukua nafasi hiyo kuanza kuangalia mtu anayeweza kuja kufaa kuwa mke. Huku wakiangalia napenda mambo gani au kama nimeshaanza kuonyesha dalili za kupenda sehemu fulani.
Nilivyopata mchumba

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA