Mamia Wajitokeza Kumsindikiza Freeman Mbowe Polisi Alipoitwa Kuhojiwa Kuhusu Kauli yake ya Maandamano…
MAMIA ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), asubuhi ya leo wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kuelekea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Mbowe amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Maoni
Chapisha Maoni