WASTARA: Starehe yangu kubwa ni Mapenzi


NIWASHUKURU wote tulioanza nao makala haya ambayo mwigizaji Wastara Juma amekuwa akifunguka kuhusiana na maisha yake, bila shaka kwa namna moja au nyingine tutakuwa tumejifunza kitu kupitia maisha yake.
Mwigizaji wa filamu Bongom, Wastara Juma akipozi.
Leo tunamalizia sehemu ya mwisho ya makala haya, tutaona jinsi gani alikutana na aliyekuwa mumewe, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Twende pamoja:
Mwandishi: Ulikutana lini na Sajuki na wapi?
Wastara: Nilikutana na Sajuki mwaka 2007 kwenye kazi ya filamu ambapo tulikuwa marafiki sana, mara nyingi tulikuwa tunakaa na kuzungumza stori za maisha huku kila mmoja akimweleza mambo aliyopitia katika mapenzi, ile filamu ilipoingia tu sokoni tukaanzisha uhusiano kwani kila mtu alikuwa na ‘stress’ za mapenzi na kila mmoja alikuwa ameshajua anachokipenda na anachokichukia mwenzake.
Wastara: Kwa hiyo uhusiano tuliuanza rasmi mwaka 2008 ambapo tulikaa mpaka 2009 ndipo tukafunga ndoa, kabla ya ndoa wakati tukiwa tunaenda kulipia ukumbi mimi na Sajuki, tulipata ajali nikavunjia mguu.
Wastara Juma akiwa na aliyekuwa mume wake marehemu, Sajuki Juma Kilowoko.
Mwandishi: Maisha ya ndoa kwa Sajuki yalikuwaje?
Wastara: Ukweli yalikuwa mazuri kwani alikuwa ni mwanaume ambaye nilikuwa namhitaji kwani alikuwa na sifa zote, alikuwa ananipenda na ananijali kwa kila kitu lakini ndiyo hivyo Mungu amemchukua.
Mwandishi: Mpaka sasa kwenye kampuni yenu (WAJEY) mna filamu ngapi?
Wastara: Tuna filamu 16 na za kushirikishwa ni 9 na nimeshirikishwa chache sababu mara nyingi Sajuki alikuwa anapenda tucheze za kwetu tu.
Mwandishi: Ni kitu gani kizuri ambacho kiliwahi kukutokea na hutakisahau maishani?
Wastara: Siwezi kusahau siku niliyopata Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike kutoka Global Publishers kupitia gazeti la Risasi kwani mpaka sasa hajawahi kutokea mwingine hivyo najiona niko bora mpaka leo.
Mwandishi: Katika maisha yako starehe yako kubwa ni nini?
Wastara Juma akiwa na meneja wake Bond Bin Sinan, ‘Bond’.
Wastara: Ukweli starehe yangu kubwa ni mapenzi kwani nikiwa na mpenzi huwa najisikia starehe na huwa ninayaheshimu sana mapenzi kuliko kitu chochote kwani yanafanya akili yangu iwe sawa hivyo hata sasa ukiona siko sawa ni kwamba sijapata mwanaume wa kunistarehesha huwa na sipendi mapenzi ya wanafunzi.
Mwandishi: Je unampenda mwanaume mwenye sifa gani?
Wastara: Nampenda mwanaume mwenye mapenzi na watoto kwani nina watoto tayari, atakayenipenda mimi kama Wastara na siyo kwa kuniona kwenye picha kwani nina ulemavu tayari pia kubwa zaidi nahitaji atakayenipa muda wake na siyo ambaye anakuwa bize na simu muda wote au kushinda mitandaoni.
Mwandishi: Je una mchumba na unatarajia kuolewa lini?
Wastara: Ukweli sina mchumba na hata sijawaza ila mume wangu Sajuki akimaliza miaka miwili tangu alipofariki dunia ndipo nitaanza kuwa na wazo la kuwa na mchumba.
Mwandishi: Vipi kuhusu huyu Bond Bin Sinan ambaye anatajwa kuwa amerithi mikoba ya Sajuki? Wastara: Hakuna yule ni mtu wa karibu yangu katika masuala ya kazi tu pia ni meneja wangu, hakuna kinachoendelea nje ya sanaa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA