Shilole akiri kutotumia Condom kwenye mapenzi
Mwigizaji
wa filamu na mwanamuziki wa miondoko ya kizazi kipya, Zuwena
Mohammed ‘Sholole’ amesema kuwa matumizi ya kondom wakati wa
mahaba hayaleti ladha ndio maana alilazimika kwenda kupima
ngoma na mpenzi wake Nuh Mziwanda ili wasiwe wanatumia kondom.
Akizungumza
na Mpekuzi wetu, Shilole alisema kuwa raha ya mapenzi ni kila
mmoja kuwa na mwenzake bila kuwa na kizuizi chenya kuondoa
ladha hiyo na baada ya kupima kila mmoja ameapa kutochepuka
ili asilite maambukizi ndani ya uhusiano wao….
“Asikudanganye
mtu, raha ya kula ndizi ni kula ikiwa imemenywa, ikiwa na
maganda inaondoa utamu ndio maaa mimi na mwenzangu tulilazimika
kwenda kupima afya zetu na kila mmoja alibainika ni mzima
hivyo tumeahidiana kutosalitiana ili tusileteane maambukizi”,alisea Shilole.
Maoni
Chapisha Maoni