FRANK AMLALAMIKIA RIYAMA KUMZIBIA RIZIKI
NYOTA wa filamu za Kibongo, Mohammed Mwikongi maarufu kama Frank,
amedai kuwa msanii mwenzie Riyama Ally anamzibia riziki kiasi kwamba
sasa anamsaka ili amweleze kitu gani aliwahi kumkosea.
Akizungumza jijini hivi karibuni, Frank alisema anamtafuta Riyama ili
aweze kumwambia ni kwa nini inakuwa hivyo kwa sababu katika filamu zote
ambazo yeye anatakiwa kucheza, mwenzake huyo huwepo na ndiye
anayependekeza watu watakaohusika na filamu hiyo.
“Tukiacha ile filamu iliyofanyika nchini Uingereza ambayo iliandaliwa
na Dida Entertainment, kuna filamu nyingine iliandaliwa na Mbunge
Shamsa Mwangunga ambaye alinipigia simu na kuniomba nicheze nafasi
aliyoipendekeza lakini baada ya siku, nafasi yangu ikachukuliwa na Slim.
Msanii wa filamu Bongo, Riyama Ally.
“Pia kuna nyingine ambayo iliandaliwa na mtu wa mtaani kwetu ambaye
ni mfuatiliaji mzuri wa kazi zetu, nafasi yangu ikachukuliwa tena na
Msungu, sasa mimi namtafuta Riyama aniambie ni kwa nini huwa ananizibia
riziki yangu wakati imeshapangwa,” alisema.
Riyama hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi kwani mara
zote iliita bila kupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno
haukujibiwa.
Maoni
Chapisha Maoni