SITTI MTEMVU, MASAA, SIKU ZINAHESABIKA KUVULIWA TAJI LAKE BILA YEYE MWENYEWE KUPENDA
WAKATI
serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema
itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu,
taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo.
Imethibitisha
kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa
katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote
kuanzia sasa.
Hata
hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa
Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo
linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu,
ambaye ni baba yake.
Imebainika
kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti
na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo
ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.
Imefahamishwa
kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na
kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa
anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi
ya miaka 18
Maoni
Chapisha Maoni