MISS TANZANIA "SITTI MTEMVU" ATOWEKA....
suala la kudaiwa kudanganya umri likiwa bado ‘bichii’, taarifa zinadai
kuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ametoweka na hajulikani
alipo, Risasi Mchanganyiko limechimbua stori kamili.
Mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Shughuli ya kumsaka mrembo huyo ili kujua undani wa sakata lake ilianzia Temeke ambako ilielezwa kuwa ndiko anakoishi.
Mapaparazi wetu walipofika katika nyumba waliyoelekezwa, walikuta
imebadilishwa na kuwa Ofisi ya Vikoba ambapo mmoja wa wahudumu wa ofisi
hiyo kwa sharti la kutoanika jina lake gazetini, aliwataka waandishi
wetu kwenda Mbezi-Makonde akidai ndiko anakoishi kwa sasa.
“Hapa ilikuwa nyumba ya zamani lakini kwa sasa ni ofisi na Sitti
hakai hapa, kama mnamtaka nendeni Mbezi-Makonde huko nasikia ndiko
anakoishi,” alisema mtumishi huyo.
Mapaparazi wetu hawakuchoka, walifunga
safari hadi Mbezi-Makonde ambapo walikuta nyumba yenye maduka
yaliyoandikwa Mtemvu Foundation, wakaenda moja kwa moja katika saluni
mojawapo iliyokuwa na bango lililosomeka Malisa huku likiwa na picha ya
Sitti sambamba na namba za simu.
Sitti Mtemvu wakati wa kutwaa taji la Miss Tanzania 2014.
Dada mmoja aliyeonekana kufanana na Sitti alizidi kutibua hali ya
hewa baada ya kusema Sitti amesafiri nje ya nchi pasipo kufafanua nchi
gani.“Sitti amesafiri nje ya nchi, ila kama mnamtaka nafikiri nitawapa
namba zake akirudi kati ya Jumatatu au Jumatano ya wiki ijayo (wiki
hii),” alisema dada huyo pasipo kutaja jina lake.
Mmoja wa majirani wa mrembo huyo alihoji inawezekanaje mrembo huyo
akasafiri nje ya nchi wakati suala lake la umri halijapata ufumbuzi?“Mh!
Ataondokaje wakati bado ana majanga ya umri?” alihoji jirani huyo.
Aidha, mapaparazi wetu hawakutaka kuishia
hapo, Jumapili iliyopita walitia timu Buza Kipera katika Kanisa la The
Revelation Church la Nabii Yaspi Bendera ambalo ilielezwa kuwa Sitti
anaabudu, ili kujiridhisha kama yupo, lakini pia hakuonekana huku
waumini wakidai hawajamuona kwa siku za karibuni.
Nabii Yaspi Bendera wa Kanisa la The Revelation Church.
“Hatumuoni siku hizi, ila alikuwa anakuja katika ibada ya peke yake
kwa nabii saa kumi lakini siku za karibuni hatumuoni,” alisema muumini
mmoja.Katika ibada inayoendeshwa kanisani hapo ambayo mapaparazi wetu
walizama ‘kiintelijensia’, Nabii Yaspi alisikika akimkingia kifua Sitti
kuwa alistahili ushindi na kumtabiria kufika mbali na hata kuwa Miss
World huku akiwaonya wanaomfuatilia mrembo huyo.
“Mara ya kwanza nilimtabiria Sitti kushinda u-miss Tanzania na kweli
akashinda, sasa wanatokea watu wakidai mara ana hipsi kubwa, ooh
kadanganya umri, huu wote ni upepo tu na utapita.“Kama Sitti
hatakengeuka kwenye imani yake atafika mbali zaidi na kushinda hata Miss
World. Wale wote watakaoendelea kumfuatilia wataparalaizi,” alisema
Nabii Yaspi.
Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), walisema bado wanalifanyia
uchunguzi suala la Ritta kudaiwa kufoji cheti cha kuzaliwa kutokana na
baadhi ya nyaraka zake kuonesha amezaliwa mwaka 1989 huku yeye akidai
amezaliwa 1991.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akitafakari jambo.
Wakati RITA na BASATA wakiwa hawajatoa tamko lolote kufuatia
uchunguzi waliodai wataufanya, gazeti hili lilifanya jitihada za
kumtafuta Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella
Mukangara ili azungumzie sakata hilo.
“Waziri ni mtu mkubwa sana kuzungumzia suala kama hilo, watafute
wasaidizi wangu pale wizarani watakuambia kinachoendelea. Naweza kutoa
tamko halafu nikaonekana mtu wa ajabu, kumbe watu wanaendelea kulifanyia
kazi, nenda kamuone Mkurugenzi wa Utamaduni atakusaidia,” alisema
Waziri huyo alipozungumza nasi kwa njia ya simu.
Maoni
Chapisha Maoni