MAAJABU HARUSI YA NYANI INDIA YATIA FORA
Zaidi ya wakazi 200 katika kijiji kimoja kaskazini mwa India wamehudhuria sherehe ya harusi ya nyani wawili.
Harusi hiyo iliandaliwa na mmiliki wa nyani hao, ambaye alisema nyani dume ni kama "mwanaye".
Sherehe
hiyo ilifanyika siku ya Jumatatu katika wilaya ya Bettiah, katika jimbo
la Bihar, huku "bi harusi" akiwa amevalia gauni maridadi.
Nyani ni viumbe wanaopendwa na watu wa jamii ya wa-Hindu.
"Bwana
harusi" ambaye anajulikana kama Ramu pamoja na mkewe mpya aitwaye
Ramdulari walipitishwa katika mitaa ya kijiji wakiwa juu ya gari
lililopambwa kwa maua na muziki ukichezwa, huku mamia ya wanakijiji
wakijipanga kuwashangilia.
Mmiliki wa nyani hao Udesh Mahto ambaye ana watoto watatu wa kiume amesema nyani Ramu ni kama mtoto wake wa kwanza.
"Nilitaka yeye ndio aanze kuoa," ameiambia Idhaa ya BBC ya Kihindi.
Bwana Mahto alimnunua Ramu kutoka Nepal miaka saba iliyopita, na baadaye kumnunua Ramdulari katika soko la kijiji.
"Mwanzoni hawakuwa wakielewana sana, lakini baadaye wakaanza kupendana, kwa hivyo nikaamua kuwafungisha ndoa," amesema.
Padre wa Kihindu Sunil Shastri "alifungisha" ndoa hiyo.
"Mwanzoni
nilikuwa na mashaka, kufungisha ndoa ya nyani, lakini nilibadili mawazo
baada ya kuona Bwana Mahto hafanyi mzaha," amesema. "Tulipanga siku na
saa ya sherehe hiyo."
Kadi za mwaliko zilichapishwa na bendi kukodishwa, huku wageni wakipatiwa makulaji.
Watu wengi kutoka vijiji vya jirani walihudhuria na wengine kupiga picha za kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.
Maoni
Chapisha Maoni