MOMBASA HALI NI TETE,MSAKO WA POLISI MISIKITINI VIJANA WANNE WAFARIKI

 KIJANA alipigwa risasi na kuuawa na wenzake zaidi ya 250 kukamatwa kwenye operesheni kali ya kusaka magaidi mjini Mombasa jana. BAADHI ya vijana waliokamatwa ndani ya misikiti ya Musa na Sakina, eneo la Majengo, Mombasa, wakati wa msako wa polisi usiku wa kuamkia jana ambapo kijana aliuawa na washukiwa zaidi ya 251 kukamatwa.Silaha mbalimbali zikiwemo gruneti, bastola, visu na mapanga zilipatikana ndani ya misikiti hiyo. Picha/LABAN WALLOGA

Akihutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Urban, mjini Mombasa, afisa mkuu wa polisi (OCPD) Mahmoud Salim, alisema kijana aliyeuawa alijaribu kushamulia maafisa wa usalama kwa gruneti walipokuwa wakiingia msikitini. “Walimpiga risasi kabla ya hajatupa gruneti hiyo na kumwua papo hapo,” akasema Bw Salim na kuapa kuwa operesheni hiyo itaendelea hadi wahalifu wote wanaswe.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA