Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Kampuni kadhaa za Marekani, zimeahidi kuwekeza dola bilioni 14 barani Afrika hasa katika sekta ya nishati na miundo mbinu. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Rais wa Marekani Barack Obama. Tangazo hilo limetolewa katika mkutano wa kwanza wa viongozi wa Afrika nchini Marekani. Mkutano wenyewe umehudhuriwa na zaidi ya marais 40 wa bara hilo. Taarifa zinazohusiana Marekani Mkutano huu unalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na mataifa ya Afrika huku China ikiendelea kuongeza uekezaji wake barani Afrika. Rais Obama pia aliandaa maankuli ya jioni kwa niaba ya marais hao katika ikulu ya White house. Mikataba hiyo iliyotangazwa Jumanne, ilijumuisha ushirikiano wa dola bilioni 5 kati ya kampuni ya Blackstone na Aliko Dangote, mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika kwa kuinua miradi ya kawi na miundo mbinu kusini mwa jangwa la Sahara pamoja na uekezaji zaidi katika miradi ya kawi in...
Maoni
Chapisha Maoni