Hakika wikiendi iliyopita ilikuwa ni shangwe tupu, lakini kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia leseni ya Chadema, Zitto Zuber Kabwe ilikuwa ya machungu pale alipojikuta akimwaga chozi ukumbini. Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia leseni ya Chadema, Zitto Zuber Kabwe akiwa na Christian Bela. Mpango mzima ulioshuhudiwa na paparazi wetu ulijiri kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Bendi ya Malaika, chini ya Christian Bella ilikuwa ikishusha burudani ya kufa mtu. Wakati Mbunge wa Jimbo la Sikonge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Said Nkumba alitesa kwenye jukwaa la Msondo Ngoma pale TTC Chang’ombe, Temeke, Zitto alifunika vibaya Mango Garden, Kinondoni, kwani alikuwa zaidi ya shabiki, pedeshee na mwimbaji. Katika muda ambao watoto wa mjini husema ni usiku mnene, Zitto ambaye yupo katika mgogoro na chama chake, alipanda jukwaani wakati prezidaa wa Malaika Band, Christian Bella ‘Obama’ akiimba wimbo wake mpya wa ‘Nani Kama Mama’ ambap...