SINEMA YA BURE LIVE: BABA WA MSANII ASHUSHA KICHAPO!
Baba huyo akizuiwa ili asiendelee kushusha kichapo hicho. Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilijiri juzikati, maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar ambapo awali binti huyo ambaye ni msanii chipukizi wa kuigiza aitwaye Jeniffer alidaiwa kupigwa mkwara na baba yake kuwa asijishughulishe na masuala ya muvi na badala yake ajikite kwenye masomo yake kufuatia tasnia hiyo kuhusishwa na skendo za ngono. Baba mmoja ambaye jina halikupatikana mara ameshusha kichapo kwa wasanii ambao ni maprodyuza waliokuwa wakimchezesha mwanaye filamu bila ridhaa yake