Waasi waunda vuguvugu dhidi ya Nkurunziza
Waasi wanaompinga
Rais Pierre Nkurunziza wameungana kuunda vuguvugu moja linalofahamika
kama The Republican Force of Burundi, na limetangaza vita dhidi ya
kiongozi huyo.
Kubuniwa kwa vuguvugu hilo kunatukia huku shinikizo kutoka kwa mataifa ya kanda hiyo, zikiongezeka.Umoja wa Afrika unaitaka serikali ya Nkurunziza ikubalie walinda amani wa Umoja wa Afrika.
Hata hivyo serikali yake imekatalia mbali ombi hilo ikidai kuwa, haiko katika hali ya mapigano yawenyewe kwa wenyewe wala hakuna hatari ya kuibuka kwa mauaji ya kimbari kwa hivyo inaichukulia jeshi hilo la kulinda amani kama jeshi la kigeni na "kikosi cha uvamizi".
Tanzania imejitokeza kupinga mpango huo wa AU wa kuwatuma wanajeshi elfu tano, wa kulinda amani wanaopangiwa kwenda Burundi, kusaidia kukomesha ghasia na umwagikaji zaidi wa damu.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga, yuko katika ziara ya kidiplomasia nchini Uganda na kisha Burundi kuhusiana na mzozo huo katika taifa hilomojawepo ya kanda ya Afrika Mashariki.
Msemaji wa serikali ya Burundi Willy Nyamitwe amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa hofu ya kuibuka kwa kundi lipya la waasi sio tishio katika serikali ya Burundi.
Nyamitwe anasema kuwa Republican Forces of Burundi, ama "Forebu" haitadumu.
''sio mara ya kwanza kwa makundi ya waasi kuibuka hapa Burundi. Tutawakanyaga mara moja''
Nyamitwe anasema kuwa Burundi ina haki ya kimsingi ya kulinda maisha na usalama wa wananchi wake na kuwa haitachelewa kuwazima mara moja.
Maoni
Chapisha Maoni