SERIKALI KUVUNJA NYUMBA HII YA SUMAYE,SOMA HAPA LIVEE


 
Sumaye matatani
 WAZIRI Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, ameingia matatani baada ya kudaiwa kuvamia eneo la wazi na kuanza kuzungushia uzio, bila kufuata sheria na utaratibu wa ujenzi.

Eneo hilo la kiwanja namba 719/1/3 lililopo Mkiocheni, mtaa wa TPDC, lilikuwa likitumika kwa ajili ya michezo, mikutano ya kisiasa, pamoja na mikusanyiko mbalimbali ya kijamii.
Kufuatia tuhuma hizo, timu ya maofi sa ardhi inachunguza uhalali wa umiliki wake, hivyo wiki ijayo majengo yaliyojengwa kwenye eneo hilo yatavunjwa, endapo ikithibitika kufanya uvamizi huo.
Mbali na Sumaye, vigogo wengine wanaodaiwa wakuvamia kiwanja hicho ni aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu Ofi si ya Rais, Philemon Luhanjo pamoja na Mbunge wa jimbo la Rungwe, Saul Amon, ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya S.H. Amon.
Awali kabla ya kuvamiwa kwa eneo hilo, ilielezwa kuwa iliyokuwa kampuni ya High Precision Technology Centre (HPTCMatsutisha), kulilinda lisivamiwe miaka ya 1970.
Hivyo mikusanyiko mbalimbali za kimichezo, pamoja na shughuli za kisiasa ilikuwa ikifanyika katika kiwanja hicho, ambako hata baada ya kampuni hiyo kufa, ililiendelea kutumika kwa shughuli za kijamii.
MAZITO YAIBUKA 
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, Sumaye anaendelea na ujenzi katika eneo hilo bila kuweka kibao chenye kuonyesha wakandarasi wanaohusika na ujenzi huo.
Lakini pia, licha baadhi ya nyaraka kudai kuwa kiongozi huyo mstaafu kulimiliki eneo hilo kuanzia mwaka 1998, hajawahi kulalamika kimaandishi kwenye uongozi wa mtaa kuhusu shughuli zilizokuwa zikiendelea kwenye eneo hilo.
Shughuli hizo ni pamoja na uongozi wa serikali ya mtaa kuweka kifusi, ili kusawazisha eneo hilo kuufanya uwanja utumike vizuri kwa ajili ya michezo.
Aidha wiki tatu zilizopita, Ofi sa Mtendaji wa Mtaa huo Mwanaidi Omary, aliongozana na mmoja ya maofi sa wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni hadi kwenye eneo hilo.
Ofi sa huyo wa ardhi alitoa notisi ya mdomo na sio ya maandishi ya kusitishwa ujenzi huo akidai mpaka mmiliki awasilishe nyaraka serikalini.
Licha ya ujenzi huo kufanyika bila kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo kutokuwepo kwa kibao kinachoonyesha mkandarasi anayehusika na ujenzi, lakini ofi sa huyo hakuchukua hatua zozote za kisheria.
Katika kutaka kujua ukweli wa mzozo huo, gazeti hili lilifanikiwa kupata barua iliyoandikwa na serikali ya mtaa kwa Halamashauri hiyo kuhoji ujenzi huo. Barua hiyo yenye kumbukumbunamba MKT/SER/MT/ TPDC/05/2015, iliyoandikwa Desemba 11, mwaka huu na kupokelewa Desemba 14, bado haijatolewa ufafanuzi na mkurugenzi kama ilivyokuwa ikielekeza.
LUKUVI KUTUMBUA JIPU
Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi, Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema serikali itavunja uzio na shughuli za ujenzi zinazoendelea kwenye eneo hilo itakapobaini ukweli, ifi kapo Jumatatu.

Katika kusisitiza hilo, Lukuvi alisema hatua hiyo itahusisha hadi vigogo wengine watakaobainika kuvamia eneo hilo.

Alisema baada ya serikali kupata taarifa, timu ya maofi sa ardhi itachunguza kwa kina eneo hilo ili kuthibitisha. Juzi gazeti hili lilishuhudia maofi sa hao wakiwa kwenye eneo hilo wakifanya uchunguzi.
 
CHANZO NA UHURU GAZETI 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA