BREAKIN NEWZZZ!!:- MBUNGE MPYA CHADEMA ATIWA MBARONI DAR
SAED KUBENEA MBARONI KWA AMRI YA MKUU WA WIYALA YA KINONDONI PAUL MAKONDA
Mbunge
wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) amekamatwa na polisi eneo la viwanda
(EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.Tukio
hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda
cha nguo cha TOOKU ambao walimpigia Mbunge wao aende kutatua mgogoro
huo.
Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha
aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na
menejimenti ya Kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.
Ilipofika
saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati
ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.
Alitoa
amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko kesho na
Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na waziri wa
Afya wanawake, jinsia na watoto.
Alimzuia
Mbunge asihutubie kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, Kubenea
alisema ni vema aseme neno, Kubenea akaanza kumdhihaki Makonda
aliyeamuru Mkutano ufungwe na akaamrisha Kubenea akamatwe mara moja kwa
lugha chafu kwa Mkuu wa Wilaya. Katika tukio hilo Mwandishi wa habari wa
Star Tv aliyekuwa anarekodi tukio hilo alinyang’anywa camera na Polisi.
Mwandishi
wa habari habari wa MwanaHALISI Josephat Isango alijaribu kumsaidia
mwenzake ili arejeshewe Camera lakini Polisi wa kituo cha Magomeni
walimtisha, na kumtaka kuondoka haraka huku wakiondoka na
aliyenyang’anywa camera.
Maoni
Chapisha Maoni