SAKATA LA MTOTO WA DIAMOND PLATINUMS NA ZARI .MAMILIONI YATENGWA...MUME WA ZARI ACHACHAMAA!
Sakata
la yule jamaa aitwaye King Lawrence, raia wa Uganda mwenye maskani yake
nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ anayedai kuwa mtoto wa staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aliyempata kupitia kwa mwandani wake,
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’
siyo wa mwanamuziki huyo, limechukua sura mpya.
KING LAWRENCE AMGEUKA IVAN
Kabla ya kutenga mamilioni hayo, King Lawrence ambaye ni rafiki wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga aliposti kwenye akaunti yake ya Instagram kile kinachoonekana ni barua ya kutaka kufanyika vipimo vya DNA ili kubaini Tiffah ni damu ya nani huku barua hiyo ikimtaja King Lawrence kuwa ndiye mhusika.
Pia kabla ya barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na kampuni ya wanasheria ya Uganda ya Web Advocates & Solicitors, King Lawrence alikaririwa akidai kwamba Tiffah ni damu ya Ivan hivyo kitendo cha kudai ni damu yake kimezidi kusababisha ‘drama’ kwenye mitandao ya kijamii.
Katika madai yake mapya, King Lawrence amebadilisha habari kuwa Tiffah ni damu ya Ivan kwa kuwa aliondoka kwa jamaa huyo akiwa tayari mjamzito na badala yake sasa yeye (King Lawrence) ndiye anadai ni baba wa Tiffah!
ADAI KULALA NA ZARI
Kwa mujibu wa King Lawrence anayedaiwa kuwa na njaa ya umaarufu, eti alilala na Zari mapema Januari, mwaka huu na kumpa ujauzito huo ambao umemleta Tiffah duniani hivyo yupo tayari kutumia gharama yoyote kumpora Diamond mtoto huyo.
ATENGA MILIONI 70
Ili kuthibitisha kile alichokisema, King Lawrence alitundika picha ya mkwanja mrefu unaokadiriwa kufikia Fedha ya Sauz takriban Randi 425,000 karibia Sh. milioni 70 za Kibongo ambazo ameapa kuzitumia kwa mawakili, wanasheria, mahakama na kwenye vipimo vya DNA kuhakikisha anammaliza Zari na kumchukua Tiffah.
AMANI LAGUNDUA KITU TOFAUTI
Wafuatiliaji wa sakata hilo wameliambia Amani kitu tofauti kwamba, kinachoonekana Ivan na King Lawrence wamepania kuhakikisha kuwa Zari na Diamond hawapati furaha ya kupata mtoto.
MUNGU AMUEPUSHE TIFFAH
Hata hivyo, hakuna chochote kinachoonekana kuwaumiza Diamond na Zari katika yote hayo yanayosemwa kwa sababu wana uhakika juu ya mtoto wao huku kila mtu akimuomba Mungu amuepushe mtoto huyo na drama za watu wasiokuwa na mshipa wa aibu.
DIAMOND AFUNGUKA
Akizungumza na Amani juu ya sakata hilo ndani ya chumba cha gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar mapema wiki hii, Diamond alifunguka kuwa, hao jamaa wanatafuta umaarufu na kwamba hakuna barua yoyote aliyopelekewa Zari.
Diamond alisema kuwa barua ya kudai mtoto wake akapimwe DNA bado haijamfikia na kama ni ishu ya kisheria inayohusu mahakama basi ingepitia kwa wakili au mwanasheria wao na siyo kupitia mitandaoni.
“Si nyumbani kwake wala ofisini kwake South wala Uganda, hakuna barua yoyote. Wewe umeona wapi mtu anaitwa mahakamani kwa barua ya kwenye ukurasa wa mtu wa social media (mitandao ya kijamii)?” Alihoji Diamond akionekana ‘kumaindi’ juu ya ishu hiyo na kuhoji: “Huyu jamaa, hivi hana kazi ya kufanya?”
AMBANA ZARI
Mkali huyo wa Ngoma ya Nana aliendelea kutiririka kuwa, alimbana Zari ambaye alimwambia hajawahi kuolewa na wao wameamua kuishi maisha yao na hawezi kufuatilia maisha ya mtu.
Alipoulizwa juu ya taarifa kwamba, King Lawrence ametenga mamilioni ili kumpora mwanaye huyo, Diamond alisema mtu huyo anatafuta umaarufu na kwamba kuna wanaomsikiliza hivyo naye anaona ndiyo njia ya kumpa umaarufu.
“Unajua kutafuta umaarufu nayo ni gharama hivyo naamini hiyo ni njia yake ya kutafuta umaarufu tu hana lolote na mimi nisingependa kujibizana na watu. Sisi tuna maisha yetu hatuna muda wa kufuatilia mambo ya watu,” alimalizia Diamond akisema kuwa mjadala huo ameufunga kwani ana uhakika Tiffah ni damu yake.
ZARI NAYE
Muda mfupi baada ya kumalizana na Diamond, Zari naye aliibuka kupitia akaunti yake kwenye Instagram ambapo alimshambulia King Lawrence kisha kumalizia kwa kumwita chizi.
“Visasi hufanywa na watu wenye akili za kitoto. Huyo mtu (King Lawrence) ni chizi,” aliandika Zari.
TUJIKUMBUSHE
Tangu Zari ajifungue Agosti 6, mwaka huu, kumekuwa na maneno mengi juu ya mtoto wake huyo wa kike ambapo kabla ya King Lawrence kudai ni mwanaye, aliyewahi kuwa mume wa Zari naye alikuwa akitajwa kama baba wa mtoto huyo hivyo wanaume hao ambao ni marafiki kuibua utata na kuonekana hawana lolote zaidi ya kutafuta umaarufu.

Maoni
Chapisha Maoni