WASIWASI WAZIDI KUTANDA IRAN VS SAUD ARABIA BAADA YA MAREKANI KUTANGAZA KUTUMA WANAJESHI

Iran has been holding military parades to mark the start of the 1980-88 Iran-Iraq war
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionIran imekuwa ikifanya maonyesho ya kijeshi katika kumbukumbu ya vita vya Iran na Iraq vya kati ya 1980-88
Rais wa Iran ameonya kuwa vikosi vya nje vinatishia usalama wa eneo la Ghuba, baada ya Marekani kusema inatuma wanajeshi katika eneo hilo.
Hassan Rouhani amesema vikosi vya nje siku zote vimesababisha 'uchungu na masikitiko' na havipaswi kutumika katika 'ushindaji wa silaha'.
Marekani inatuma wanajeshi zaidi Saudi Arabia baada ya shambulio dhidi ya vituo vyake vya mafuta, hatua ambayo mataifa yote mawili yanaishutumu Iran kutekeleza.
Rouhani amesema pia kwamba Iran itawasilisha mpango mpya wa amani wa Ghuba kwa Umoja wa mataifa katika siku zijazo.
Mwaka huu, kumeendelea kushuhudiwa uhasama baina ya Marekani na Iran, kufuatia hatua ya rais Donald Trump kujitoa katika Donald Trump kujitoa katika makubaliano ya nyuklia yalionuiwa kudhibiti shughli za Iran za nyuklia ili kwa upande wake ipunguziwe vikwazo.
Hatua ya hivi karibuni iliyozusha joto inatokana na mashambulio ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya vituo vya mafuta vya Saudi Arabia huko Abqaiq na Khurais mnamo September 14.
Waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulio hilo, lakini Marekani na Saudia zinasema Iran ndio iliohusika, kauli ambayo Tehran inaipinga vikali.
Rouhani amesema nini?
Alikuwa akizungumza katika kumbukumbu ya kuanza kwa vita vya Iran - Iraq vya mnamo 1980-1988 pamoja na maonyesho ya kijeshi yaliokuwa yakifayika mjini Tehran na katika miji mingine.
Hassan Rouhani said foreign forces had always brought "pain and misery"Haki miliki ya pichaEPA
Image captionHassan Rouhani amesema vikosi vya nje siku zote vimesababisha 'uchungu na masikitiko'
"Vikosi vya nje vinnaweza kuzusha matatizo na ukosefu wa usalama kwa watu wetu na eneo letu," alisema katika hotuba ya taifa iliyopeperushwa kwenye televisheni.
Ametaja kutumwa kwa vikosi hivyo katika siku za nyuma kama janga na amewaambia wanajeshi hao 'wakae mbali'.
"Kwa ni wakweli, basi wasilifanye eneo leu kuwa ni sehemu ya ushindani wa silaha... munavyozidi kukaa mbali na maeneo na mataifa yetu ndipo kunapozidi kuwa na usalama zaidi."
Vipi kuhusu mpango wake wa amani?
Rais huyo amesema mpango huo wa amani utawasilishwa kwa Umoja wa mataifa, unaoanza vikao vya baraza kuu mjini New York Ijumanne.
Hatahivyo, hakutoa taarifa akisema tu kwamba amani katika mfereji wa Hormuz inaweza kufikiwa "kwa ushirikiano wa mataifa tofauti".
Rouhani amesema Iran "ipo tayari kuachana na makosa ya zamani" yaliotekelezwa na majirani wa kieneo.
"Katika wakati huu muhimu wa kihistoria tunawatangazia majirani zetu kwamba tunanyoosha mkono wa urafiki na undugu kwao," amesema.
Waasi wa Houthi nchini Yemen pia wamependekeza mpango wa amani wakisema watasitisha mashambulio yote dhidi ya Saudi Arabia ili muradi ufalme huo na washirika wake wafanye vivyo hivyo.
Mjumbe maalum wa Marekani nchini Yemen Martin Griffiths amesema katika taarifa ni muhimu "kuitumia fursa hii na kusogea mbele kwa hatua zote kupunguza ghasia, hatua za kijeshi na majibizano yasiosaidia".
Map showing who supports whom
Nini maaa ya kutumwa vikosi vya Marekani?
Wizara ya ulinzi Marekani ilitangaza Ijumaa kufuatia ombi la Saudia , kwamba watatumwa wanajeshi wa kiasi fulani katika ufalme huo, sio maelfu na watakaoshughulika na mfumo wa ulinzi wa angani na wa makombora.
Waziri wa ulinzi Mark Esper amesema: "Tutashirikiana kushinikiza kuwasilishwa kwa vifaa vya kijeshi."
Tangazo hilo limechangia muitikio mkali kutoka kwa jeshi la Iran Revolutionary Guard IRGC - kitengo cha juu cha jeshi Tehran kilichotambuliwa na Marekani kama kundi la kigaidi.
Kamanda meja Jenerali Hossein Salami amesema: "Yoyote anayetaka ardhi yao kugeuka eneo la mapambano, endelea. Jihadhari, uchokozi mdogo hautosalia kuwa mdogo. Tutamuandama mchokozi yoyote."

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA