Shambulio la vituo vya mafuta Saudia: Akiba ya mafuta Marekani iliyofichwa kwenye mapango ya chini
Kufuatia mashambulio katika vituo vikuu vya mafuta Saudi Arabia, maafisa nchini Marekani wamekuwa wakizungumza kuhusu kutumia akiba kubwa ya mafuta iliyofichwa nchini humo.
Wakati bei ya mafuta ikipanda, rais Donald Trump alituma ujumbe kwamba wanaweza kutumia mafuta " kuhakikisha usambazaji upo sawa katika masoko".
Mafuta aliyokuwa akiyataja ni takriban mitungi milioni 640 iliyowekwa katika mapango ya chumvi ya chini katika majimbo ya Texas na Louisiana. Fikra ya kuweka akiba hii ilitokea katika miaka ya 1970.
- Marekani yasema Iran iliishambulia Saudia
- Mafuta yapanda bei baada ya mashambulio Saudia
- Kwanini Saudia na Iran ni maadui wakubwa?
Washirika wote wa shirika la kimataifa la nishati ni lazima waweke akiba iliyo sawa na mafuta yanayoweza kutumika kwa siku 90, lakini akiba ya Marekani ndio iliyo kubwa ya dharura duniani.
Kwanini iliidhinishwa?
Wanasiasa wa Marekani walikuja na fikra hiyo ya kuweka akiba ya mafuta kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1970 baada ya marufuku ya mafuta ya mataifa ya mashariki ya kati kuchangia bei kupanda sana kote duniani.
Washirika wa shirika la mataifa ya kiarabu yanayosafirisha mafuta - zikiwemo Iran, Iraq, Kuwait, Qatar na Saudi Arabia - yalikataa kuiuzia Marekani mafuta kwasababu inaiunga Israel mkono katika vita kati ya mataifa ya kiarabu na Israeli mnamo 1973.
Vita hivyo vilidumu kwa wiki tatu hadi Oktoba mwa huo. Lakini marufuku iliyoyalenga mataifa mengine pia - iliendelea hadi Machi 1974, na kusababisha bei kupanda nara nne zaidi duniani kutoka $3 hadi takriban $12 kila mtungi.
Picha za magari yakiunga foleni katika vituo vya kujaza mafuta katika baadhi ya mataifa yalioathirika zilitapakaa na kudhihirisha ukubwa wa mzozo huo.
Bunge la Marekani likapitisha sheria ya sera ya nishati na uhifadhi ya 1975. Iliidhinisha akiba ya kimpango ya mafuta itakayotumika iwapo kutashuhudiwa tatizo jingine kubwa la usambazaji.
Akiba hiyo ni nini?
Kufikia sasa kuna sehemu nne ambako mafuta yanahifadhiwa: karibu na Freeport and Winnie jimboni Texas, na nje ya Lake Charles na Baton Rouge huko Louisiana.
Kila eneo lina mapango ya chumvi yalioundwa yalio na ureuf wa kilomita moja moja kushuka chini ambako mafuta yanahifadhiwa. Hii haigharimu pakubwa ikilinganisha na kuyahifadhi katika matanki juu ya ardhi na pia ni salama - kemikali iliomo kwenye chumvi na shinikizo la chini ya ardhi linayazuia mafuta kutovuja.
Eneo kubwa zaidi huko Bryan Mound karibu na Freeport lina uwezo wa kuhifadhi takriban mitungi milioni 254 ya mafuta.
Mtandao wa akiba ya mafuta hayo unasema kwamba mnamo Septemba 13 kulikuwa na mitungi milioni 644.8 ya mafuta ndani ya mapango hayo.
Kwa mujibu wa afisi inayotoa taarifa kuhusu nishati Marekani, Raia wa nchi hiyo walitumia mitungi milioni 20.5 ya mafuta kwa siku mnamo 2018 - ina maana kwamba kna mafuta ya kutosha kuliendesha taifa hilo kwa kiasi ya mwezi mmoja.
Imeratibiwa vipi?
Kwa mujibu wa sheria hiyo ya mnamo 1975 iliosainiwa na Gerald Ford, rais anaweza kuidhinisha kutumika kwa akiba iwapo tu kunashuhudiwa 'matatizo makubwa ya usambazaji'.
Matatizo ya kiufundi ina maana kwamba ni kiasi kidogo tu kitakachoweza kutumika kutoka kwenye mapango kila siku, kumaanisha kwamba hata iwapo kuna agizo la rais kutumia mafuta hayo, huenda ikachukua wiki mbili mpaka mafuta hayo yatafika katika masoko.
Zaidi ya hayo, mafuta hayo hata hayajasafishwa. yatahitaji kushughulikiwa kugeuzwa ya kutumika kablaya kuweza kutumika kwenye magari, meli na hata ndege.
Waziri wa nishati Marekani Rick Perry ameiambia CNBC Jumatatu kwamba ni "mapema kidogo" kuanza kuzungumza kuhusu kutumia akiba kufuatia mashambulio hayo dhidi ya vituo vya mafuta Saudi Arabia.
Yameshawahi kutumika awali?
Yalitumika mwisho mnamo 2011, wwakati kulishuhudiwa matatizo ya usambazaji yaliotokana na wimbi la maandamano katika ulimwengu wa kiarabu na kuchangia nchi wanachama wa IEA kuruhusu kutumika jumla ya mitungi milioni 60 ya mafuta kupunguza matatizo yalioshuhudiwa kwa usambazaji nishati.
Hatahivyo, Marekani imeuza kiasi kikubwa cha mitungi ya mafuta mara kadhaa.
Rais George H W Bush aliidhinisha matumizi ya akiba hiyo wakati wa vita vya ghuba mnamo 1991, huku mwanawe George W Bush aliruhusu kuuzwa kwa mitungi milioni 11 kufuatia kimbunga Katrina.
Lakini manufaa ya kuweka akiba hiyo kubwa wakati ambapo uzalishaji nishati Marekani umeimarika umehojiwa. baadhi huko Washington wamewahi pia kupendekeza kuiondoa akiba hiyo kabisa.
Ripoti ya uwanjibikaji wa serikali ilipendekezo hilo mnamo 2014, ikisema itachangia kushuka kwa bei ya mafuta katika vituo kwa manufaa ya watumiaji nchini . Mnamo 2017 utawala wa Trump ulijadili kuuzwa kwa nusu ya akiba hiyo kusaidia kukabiliwa na nakisi ya serikali.
Chini ya utawala wa rais Bill Clinton, mitungi milioni 28 iliuzwa mnamo 1997 kama sehemu ya hatua ya kupunguza nakisi ya serikali.
Maoni
Chapisha Maoni