TOBO KATIKA PAA LA DUNIA’ limekuwa dogo kuwahi kushuhudiwa katika miongo mitatu!
Tobo katika paa la dunia juu ya bara la kusini duniani Antarctica huenda limekuwa dogo mno mwaka huu katika miongo mitatu, wasayansi wanasema.
Uangalizi wa viwago vya juu vya gesi katika anga umeashiria kuwa kwamba tobo halijafunguka mwaka kama inavyofanyika kawaida.
Kituo cha uangalizi cha Umoja wa Ulaya cha Copernicus Atmosphere Monitoring Service (CAMS) kinasema kwa sasa kimefikia nusu ya eneo jumla linaloonekana kufikia Septemba kati.
Tobo hilo pia halipo katikati na li kando na eneo hilo la kusini shirika hilo la EU linaongeza.
Wataalamu wa CAMS' waliopo Reading nchini Uingereza wanatabiri vinwaog vilivyoimarika vya ozoni au kuongezeka kwa wastani katika siku zijazo.
Ozoni ni molekuli inayojumuisha atomi tatu za hewa safi ya Oxygen. Inatumika kuchuja miale ya sumu kutoka kwenye jua.
Gesi inaundwa mara kwa mara na kuharibiwa katika anga ya stratosphere, kiasi ya 20-30km juu ya dunia.
Katika anga ambayo haina uchafuzi, mzunguko huu wa utengeenzaji na uharibifu upo katika mizani sawa. Lakini kemikali zilizo na chlorine na bromine zinazotokana na shughuli za binaadamu zimeigeuza mizani upande mmoja na kusababihsa kupotea kwa ozoni ambayo ipo kwa kiwango kikubwa katika Antarctic baina ya Septemba na Oktoba.
Azimio la Montreal liliosainiwa na serikali tofuati mnamo 1987 lilijaribu kuishughulikia hali kwa kupiga marufuku utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazosababihsa uharibifu.
Katika wiki iliyopita, kumekuwa na mfuniko mwembamba katika umbali wa kilomita milioni tano mraba. wakatikama huu mwaka jana ilikuwa ni katika eneo la zaidi ya kilomita milioni 20 mraba licha ya kwamba mnamo 2017 ilikuwa ni zaidi kidogo ya kilomita milioni 10 mraba.
Kwa maneno mengine kuna utoafuti mzuri wa kiwango kutoka mwaka mpaka mwaka.
Hali hiyo hutokea kila mwaka wakati Antarctic inapotoka katika majira ya baridi. Utaratibu unaofanya kazi kuharibi ozoni katika anga ya stratosphere ilio baridi huidhinishwa kwa kurudi jua katika latitudi za juu.
Wanasayansi wanasema kwamba wakati kumeshuhudiwa hasara mapema kuliko ilivyotarajiwa mwaka huu, ilipunguzwa kwa ujoto uliochangia kupanda kwa nyuzi joto katika anga ya stratosphere kwa takriban nyuzi joto 20-30 .
Hii iliathiri mfumo wa uharibifu wa ozoni.
Richard Engelen ni naibu mkuu wa CAMS. Anasema kiwango kidogo kinachoonekana kufikia sasa mwaka huu inatia moyo lakini anaonya kuhusu kurudi nyuma kutokana na kutosheka na hali iliopo.
"Nadhani hivi sasa tunapaswa kuliangalia hili kama tatizo zuri. Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu nini kilichosababisha hali hii." ameiambia BBC News.
"Halihusiki tu na azimio la Montreal ambapo tumejaribu kupunguza chlorine na bromine angani kwasababu bado zipo. Inahusu zaidi tukio muhimu. Watu bila shaka watauliza maswali yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini hatuwezi kulijibu hilo kwa sasa."
CAMS ni shirika linaloendeshwa na Umoja wa Ulaya la European Centre for Medium-range Weather Forecasts (ECMWF).
Taarifa yao imejumuishwa na mifano ya hali inayodhihirika angani.
Shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani World Metrological Organization-lilidhamini ukaguzi wa mnamo 2018 wa sayansi wa kupungua kwa Ozoni na kusema huenda kuimarishwa kwa zozni kurudi viwango vya awlai vya mwaka 1970 huenda kukadhihirika takriban mwaka 2060.
Maoni
Chapisha Maoni