NI MATAIFA GANI AFRICA YANATUMIA NISHATI YA NYUKLIA NA KWANINI?

South Africa currently has one nuclear plant
Haki miliki ya picha
Uganda imesaini makubaliano na Urusi kuisaidia kujenga uwezo wake wa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya kutengeneza nishati, dawa na matumizi mengine ya amani.
Hatua hii inafuata kusainiwa kwa makubaliano mnamo mei mwaka jana baina ya serikali ya rais Yoweri Museveni na shirika la kitaifa la nyuklia China CNNC, kulisaidia taifa hilo la Afrika mashariki kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya amani.
Katika ujumbe rasmi wa wizara ya nishati Uganda, makubalinao hayo na Urusi yalisainiwa hapo jana Jumatano huko Vienna kati ya waziri Irene Muloni na naibu mkurugenzi mkuu wa shirika la kitaifa la nishati ya atomiki ROSATOM, Nikolai Spasskiy.
Urusi itaisaidia Uganda kujenga miundo mbinu ya nyuklia kwa matumizi katika viwanda sekta ya afya na pia ukulima.
"Spasskiy ameeleza uwajibikaji na utayari wa ROSATOM kuisaidia Uganda kuidhinisha matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia hususan katika ujenzi wa kinu cha nishati ya nyuklia," taarifa imeeleza.

Afrika inasonga mbele katika matumizi ya nishati ya nyuklia

Kwa mujibu wa ripoti ya IAEA ya mwaka 2015, zaidi ya nchi 30 duniani, theluthi moja zikitoka Afrika zinajiandaa kuanzisha mipango ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa usaidizi wa wataalamu kutoka shirika hilo.
Kampuni ya Urusi Rosatom, imeshauriana na kuingia katika mikataba ya makubaliano na serikali kadhaa barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni katika kuidhinisha matumizi ya nishati ya nyuklia.

Rwanda:

Mwaka jana kampuni hiyo ilitangaza kwamba imesaini makubaliano (MOU) na serikali ya Rwanda kupitia wizara yake ya miundo mbinu kushirikiana katika matumizi ya amani ya nishati ya atomiki.
Makubaliano hayo yaliidhinishwa kwa misingi ya ushirikiano wa pande mbili kujenga miundo mbinu ya nyuklia Rwanda na miradi mingine inayotokana na teknolojia ya nyuklia kama ilivyo kwa Uganda hivi sasa katika sekta zikiwemo za afya na hata ukulima.

Kenya:

Katika nchi jirani Kenya, serikali na kampuni hiyo ya Urusi zilisaini maelewano mnamo 2016 ya matumizi ya amani ilio kutoa fursa ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili ya matumizi ya nyuklia.
Katika kuhimiza ushirikiano huo, mwaka jana Rosatom ilishiriki katika warsha ya mafunzo nchini Kenya - Kenya Bureau of Standards 3rd Radiation Protection Safety and Security Training programme.
Katika warsha hiyo afisa mkuu mtendaji wa Rosatom, Dmitry Shornikov alieleza kwamba mataifa mengi ya Afrika yanaelekea katika matumizi ya nishati ya nyuklia kuweka usawa wa matumizi ya nishati na kukabiliana nchangamoto katika upatikanaji wa nishati.
"Nishati ya nyuklia inaweza kutegemewa, ina gharama ya kumudu na haina madhara na nishati inayotokana na chanzo kisichokuwa na athari kwa mazingira." alisema Shornikov.
Kenya imesema kwamba itaendelea na mpango wake wa kuhakikisha kwamba ina kiwanda cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia kufikia 2027.
Kaimu afisa mkuu mtendaji wa kukinga dhidi ya miali nururishi nchini Kenya Joseph Maina amesema Wakenya hawafai kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia.
"Kumekuwa na ajali tatu pekee kubwa za nyuklia katika historia. Kisiwa cha Three Mile Marekani, 1978; Chenorbyl nchini Ukraine, 1986 na Fukushima nchini, Japan, 2011. Usalama umeimarishwa kutokana na mafunzo kutoka kwa mikasa hiyo," amesema.
Kenya imekuwa na mpango wa kuzalisha kawi ya nyuklia kwa muda.
Picha ya kiwanda cha kuzalisha kawi ya nyuklia cha Cattenom mashariki mwa UfaransaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionPicha ya kiwanda cha kuzalisha kawi ya nyuklia cha Cattenom mashariki mwa Ufaransa

Afrika kusini

Afrika kusini ina vinu viwili vya nyuklia vinavyozalisha 5% ya nishati ya umeme nchini.
Kwa mujibu wa shirika la nyuklia duniani kinu cha kwanza cha nyuklia katika taifa hilo kilianza kuhudumu mnamo 1984.
Kinu cha Koeberg kilijengwa na Framatome (ambao sasa inafahamika kama Areva). Kinamilikiwa na kampuni ya kusambaza umeme nchini humo Eskom.
Urusi imetia saini mkataba wa kujenga viwanda viwili vya nishati ya nyuklia nchini Nigeria huku taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika likiweka mikakati ya kumaliza matatizo yake ya umeme.
Image captionUrusi imesaini mkataba wa kujenga viwanda vya nishati ya nyuklia nchini Nigeria huku taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika likiweka mikakati ya kumaliza matatizo yake ya umeme.

Nigeria

Taifa lililopo Afrika magharibi Nigeria limesaini makubaliano na Urusi kuidhinisha ujenzi wa vinu vinne vya nishati ya nyuklia na taasisi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia nchini.
Tume ya nishati ya atomiki nchini Nigeria (NAEC) imesaini makubaliano na kampuni hiyo ya Urusi Rosatom, mnamo 2016 kando kando mwa mkutano wa kimataifa wa atomiki, ATOMEXPO 2016 mjini Moscow.
Dhamira ya kuidhinishwa makubaliano hayo ni miongoni mwa mengine, kuimarisha mfumo duni wa nishati nchini na kuweka mikakati ya kumaliza matatizo yake ya umeme.
Hatahivyo tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo, kumeshuhudiwa shutuma zinazogusia zaidi na kutahadharisha kuhusu hatari za nyuklia , miongoni mwa mengine.
Vinu hivyo vinavyotarajiwa kujengwa na Rosatom, vinatarajiwa kugharimu takriban $80billion, huku cha kwanza kikitarajiwa kukamilika kufikia 2025.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA