Ukungu wasababisha anga Indonesia kugeuka rangi nyekundu
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Anga katika jimbo moja nchini Indonesia iligeuka nyekundu mwishoni mwa juma, kutokana na moto wa msituni uliosambaa katika sehemu kubwa za nchi.
Mkaazi mmoja katika jimbo la Jambi, aliyepiga picha za anga hiyo amesema ukungu uliotokana na moshi huo "ulimuumiza macho na koo".
Kila mwaka, moto nchini Indonesia husababisha ukungu wa moshi unaoweza kulifunika eneo zima la kusini mashariki mwa Asia.
- Picha: 'Sekunde kadhaa kabla ya ajali ya ndege'
- Afariki akimkwepa ndege mwenye hasira
- Kiboko cha mbu wa malaria chapatikana
Mtaalamu wa utabiri wa hali ya hewa ameiambia BBC rangi hiyo ya anga imetokana na hali isiyo ya kawaida inayofahamika kama Rayleigh scattering.
Eka Wulandari, kutoka kijiji cha Mekar Sari jimboni humo Jambi alipiga picha za anga hiyo yenye wekundu mithili ya rangi ya damu katika msururu wa picha zilizopigwa mwendo wa saa sita mchana siku ya Jumamosi.
Mkaazi huyo mwenye umri wa miaka 21, alituma picha kwenye mtandao wa Facebook. Kufikia sasa picha hizo zimesambazwa zaidi ya mara 34,000.
Lakini ameiambia BBC Indonesian kwamba watu wengi walitilia shaka ukweli wa picha hizo.
"Lakini ni kweli. Ni picha na video halisi nilizopiga kwa simu yangu," alisema, akiongeza kwamba ukungu huo ulisalia pakubwa siku ya Jumatatu.
Mtu mwingine aliweka video kwenye twitter ilioonyesha anga hiyo nyekundu.
"Hii sio sayari ya Mars. Hii ni Jambi," alisema Zuni Shofi Yatun Nisa. "Sisi binaadamu tunahitaji hewa safi, sio moshi."
Ruka ujumbe wa Twitter wa @zunishofiyn
Ini sore bukan malam. Ini bumi bukan planet mars. Ini jambi bukan di luar angkasa. Ini kami yang bernafas dengan paru-paru, bukannya dengan insang. Kami ini manusia butuh udara yang bersih, bukan penuh asap.
Lokasi : Kumpeh, Muaro Jambi #KabutAsap #KebakaranHutanMakinMenggila
46.2K people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zunishofiyn
Ukungu huo unaotokana na moto wa misitu ni mbaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka kadhaa.
Unatokana na kuteketea kwa misitu Indonesia na kwa kiasi kidogo , katika sehemu za Malaysia.
Moto huo hushika kasi ifikapo Julai hadi Oktoba wakati wa msimu mkavu Indonesia.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la kupambana na majanga Indonesia, takriban hekari 328,724 za ardhi ziliteketea katika miezi minane ya mwaka huu.
Mashirika makubwa na wakulima wadogo ndio wanaolaumiwa kwa moto huo kutokana na kupatiliza fursa ya majira ya ukavu kusafisha mashamba ili kuyatayarisha kwa ukulima.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni