LISA LI: NYOTA MASHUHURI FEKI, AUMBUKA BALAAAA!
Mshawishi maarufu wa mtandao nchini China ameangaziwa kwa kuishi maisha ya "uwongo", baada ya mwenye nyumba aliyopangisha kufichua maisha yake halisi yanayotofautiana na muonekana anaonadi mtandaoni.
Kanda ya video iliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha nyumba ya Lisa Li - Mwanablogu maarufu aliye na mashabiki milioni 1.1 - ikiwa na uchafu uliozagaa kila sehemu- ikiwa ni pamoja na vyakula vilivyooza na kinyesi cha mbwa.
- Kwa nini Marekani inapoteza uwezo wake wa kijeshi dhidi ya China na Urusi?
- Ushahidi mpya wamuweka 'pabaya' Trump
- Wapiganaji wa Majimaji kujiunga na jeshi DR Congo
Tangu kanda hiyo iliposambazwa mitandaoni Bi Li ameomba msamaha.
Kwanini Bi Li ni mashuhuri?
Lisa Li anafahamika China kama "wang hong", ama "Mtu mashuhuri", katika mtandao maarufu wa Sina Weibo.
Akaunti yake, sawa na ya vijana wa Kichina ambao ni watu mashuhuri wa mtandaoni, inaonesha jinsi anavyopenda starehe kwa kusafiri katika maeneo ya kuvutia, kuhudhuria hafla tofauti na kula vyakula vya hali ya juu.
Lakini tangu mwenye nyumba aliopanga kumuanika mtandaoni amepata umaarufu mwingine tofauti kabisa (maisha yake ya faraghani ambayo ameweka siri).
Mwenye nyumba alifanya nini?
Baada ya Lisa Li kupuuza simu alizompigia, mamilioni ya watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Weibo walimtazama mwenye nyumba aliyetajwa na vyombo vya habari kama Bi Chen, akioneshana mazingira machafu ya nyumba ya Lisa.
Bi Chen aliiambia Pear Video kuwa hata wataalamu wa kufanya usafi wamekataa kusafisha nyumba hiyo na kuongeza kuwa mpangaji alikuwa anadaiwa maelfu ya yuan ambazo hajalipa kupata huduma muhimu wanazopewa wapangangaji wengine.
Chen amesema hakua na budi kupiga ripoti polisi ili kukoa mali yake na kupata fedha anazoda.
Lakini Chen alipata umaarufu baada ya kuonesha ukurasa wa Weibo wa mpangaji wake kwa kituo hicho, akisema: "Huyu ni mtu mashuhuri sana mtandaoni na anafuatiliwa na watu milioni moja."
Aliaimbia Pear Video katika mahojiano ya kipekee akisema "mwanamke mrembo" lakini muonekano wake ni tofauti na "uvundo" na uchafu uliopo nyumbani kwake.
Bi Li amesemaje?
Baada ya mamiliaoni ya watu kuona kanda ya video ya nyumba hiyo Bi Li alijitokeza na badala ya kutoa taarifa katika mtandao wa kijamii aliamua kukutana na mwenye nyumba ana kwa ana na kuomba msamaha.
"Nakubali nimekosea kutokana na tukio hili," alimwambia Bi Chen. Alinaswa katika kanda ya video akimsalimia mwenye nyumba.
Alielezea sababu za kutokuwepo kwake katika mtandao maarufu wa habari -The Paper, akisema ilitokana na kazi nyingi.
Pia alisema alikuwa mgonjwa na alipotoka hospitali alienda safari ya kikazi.
Aliongeza kuwa hivi karibuni alipokea ujumbe mwingi katika WeChat na huenda hakuona ya mwenye nyumba.
"Sasa nitasafisha … nitapasafisha usiku huu," aliiambia The Paper.
Mashabiki wa Bi Li wanasemaje?
Kanda inayomuonesha Bi Li akizoa kinyesi cha mbwa kwa kutumia kifagio cha nyumbani imewagutusha mashabiki wake huku baadhi yao wakimkejeli mtandaoni.
Zaidi ya watumiaji 60,000 wametoa maoni katika ukurasa wake, na wengi wao wamesema wataacha kumfuatilia huku wakiimuita "feki".
Baadhi yao pia wamehoji ukweli wa mahajiano yake katika vyombo vya habari.
Mashabiki wake pia wamegundua kuwa amebadilisha anuani yake katika mtandao wa kijamii na kufuta posti za awali.
Hii sio mara ya kwanza visa kama hivi vinashuhudiwa nchini China.
Taifa hilo limekua likiwashinikiza raia wake mashuhuri kuwajibika katika jamii.
Mwezi Julai vlogger mmoja raia wa China alikejeliwa sana mitandaoni baada ya hitilafu ya kimitambo wakati akifanya live-stream( matangazo ya moja kwa moja mtandaoni) kumuonesha kuwa mwanamke wa wa umri wa makamo tofauti na jinsi alivyojinadi mtandaoni kuwa mwanamke kijna.
Baadhi ya watu mashuhuri mtandaoni walikiuka "maadili" wamefungwa jela kwa muda mfupi.
Mwezi Oktoba mwaka 2018, Yang Kaili, kinara mashuri wa live-stream aliye na mamiliaoni ya mashabiki, alizuiliwa kwa siku tano kwa kukashifu wimbo wa taifa.
Mtandao Huya wa kupeperusha matangazo ya moja kwa moja mtandaoni ulifuta tangazo hilo na kumpiga marufuku,ukisema kuwa mitandao ya kurusha matangazo yanastahili kuzingatia sheria kikamilifu.
Maoni
Chapisha Maoni