‘Mwakyembe Akianza Mchakato wa Katiba Tu, Nitafunguka’ Warioba
Urafiki wa Jaji Joseph wariona na chama chake cha CCM uliofufuka wakati wa Uchaguzi Mkuu, unaweza kuingia tena doa baada ya waziri huyo mkuu wa zamani kusema iwapo Serikali itaanza harakati za kumalizia mchakato wa Katiba, atatoa yake ya moyoni. Jaji Warioba, aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alishambuliwa na makada wa chama hicho kutokana na kuwasilisha Rasimu ya Katiba iliyotofautiana na utashi wa CCM, hasa kwenye suala la muundo wa Muungano kuwa wa serikali tatu. Lakini tofauti hizo zilipotea wakati wa Uchaguzi Mkuu alipoamua kusimama kidete kumtetea mgombea urais wa CCM bila ya kujali kilichomsibu kwenye Bunge la Katiba. Baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kueleza kuwa Rais John Magufuli amemuagiza aendelee na mchakato wa Katiba kuanzia pale alipoishia, Jaji Warioba amehifadhi maoni yake, lakini anasema ana yake ya moyoni. “Kwa sasa siwezi kusema chochote kuhusu kauli ya Serikali kuendelea na mchakato wa Kat...