WANASAYANSI WALIDHANI SAYARI HII HAIKUWEPO!
Wataalam wa anga wamegundua sayari kubwa ambayo wanasema, haipaswi kuwepo, kulingana na nadharia za sasa. Ulimwengu huo unaofanana na sayari ya Jupita ni mkubwa sana ikilinganishwa na nyota yake mwenyeji, hatua inayokinzana na wazo kuhusu jinsi sayari zinavyoundwa. Nyota hiyo ilio umbali wa kilomita trilioni 284 , ni ya aina nyekundu na ndogo - ambayo ni aina ya kawaida katika galaxy yetu. Marekani yawatahadharisha raia wake wanaolekea Tanzania Mwanamfalme Harry atembea katika eneo la mabomu yaliotegwa ardhini Je wajua kwamba alama hii sasa ni ya chuki? Kundi la kimataifa la wataalam wa angani limeripoti matokeo yake katika jarifda la sayansi duniani. ''Inafurahisha kwa sababu tumejiuliza kwa muda mrefu kama iwapo sayari kubwa kama Jupita na Saturn zinaweza kunda nyota ndogo kama hizo," alisema Profesa Peter Wheatley, wa Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza, ambaye hakuhusika na utafiti wa hivi karibuni "Nadhani maoni ya jumla yalikuwa kwamba sayari h...