Shela ya Harusi Aliyovaa Nancy Summary Siku ya Harusi Yake Yazua Gumzo
Shela alilovaa Miss Tanzania 2005, Nancy Abraham Sumary alipokuwa akifunga ndoa na mchumba’ke, Lucas Neghesti mwishoni mwa wiki iliyopita, limezua gumzo kutokana na ‘usimpo’ wake licha ya gharama yaku kuwa kubwa ambapo linadaiwa kununuliwa kwa shilingi milioni tano za Kitanzania.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kisa cha kuzua gumzo ni jinsi lilivyokuwa simpo kwa muonekano ingawa lilimpendeza na kumtoa chicha kwani wapo waliopenda namna lililofanana na lile la mdogo wake staa wa muziki Marekani, Beyonge Knowles, Solange Knowles ambalo ndiyo lilitakiwa kuwa na gharama kubwa kwani linastahili kutokana na kuwa limeshavaliwa na staa huyo wa Marekani.
Hata hivyo, wapo waliomsifia kwa jinsi alivyojidizaini na kuwa bibiharusi simpo na mwenye muonekano wa kimataifa kwani kwa Watanzania wengi imekuwa ni vigumu mwanamke kufunga ndoa akiwa na nywele zake (natural) tofauti na wengine ambao hupenda matashtiti kibao.
Nancy na Luca walifunga ndoa Ijumaa iliyopita ambapo mrembo huyo alivaa kikofia kilichodizainiwa na mwanamitindo mfaransa na fasheni yake ni ya mwaka 2016 huku mumewe akivalishwa na mwanamitindo, Martin Kadinda
Maoni
Chapisha Maoni