Bodi ya Mikopo yatangaza majina 1,091 ya wadaiwa Ambao Hawataki Kulipa (Awamu ya kwanza).....Bonyeza Hapa Ujitazame Kama na Wewe Jina Lako Lipo


Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB), inawaarifu wadaiwa wote ambao mpaka hivi sasa hawajaanza kulipa mikopo waliochukua kipindi wanasoma, na wenye majina yao kwenye orodha hii kwamba wamevunja mkataba kutokana na sheria ya bodi hiyo No. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) sehemu ya 19 (1).

Na wanataarifiwa kwamba, kulingana na sheria hiyo ya bodi (HESLB)  No. 9 ya 2004, Bodi imedhamiria kutenda yafuatayo:-

(i) Bodi itachukua hatua za kisheria kulingana na kipengele cha 19 (a) (1) cha sheria ya bodi.

(ii) Mdaiwa atapewa penati ya 5%  juu ya ile 5% iliyokua ikitozwa kabla kwa kila mwezi kwenye deni lililobakia au alilonalo.

(iii) Mdaiwa ataongezewa gharama za kumtafuta alipo ili alipe deni zilizoingiwa na bodi.

(iv) Mdaiwa atawekwa kwenye ‘blacklist’ na maelezo yake yatapelekwa  kitengo cha kumbukumbu ya wakopaji na hivyo kushindwa kukopa sehemu nyingine yoyote.

(v) Mdaiwa atazuiliwa kupata udhamini wa Serikali au udahili wa masomo ya juu kwenye vyuo vyovyote ndani na nje ya nchi.

(vi) Maelezo yao yatapelekwa kwenye Wizara ya mambo ya ndani, kitengo cha Uhamiaji na balozi zote ambako watakataliwa safari zozote za kwenda nje ya nchi.

Wadaiwa wote ambao majina yamechapishwa kwenye magazeti na kwenye tovuti ya bodi ya mikopo (Bonyeza hapa kuyasoma majina hayo) wanatakiwa kulipa madeni yao mapema iwezekanavyo kuzuia wao kupata adhabu hizo zilizotajwa hapo juu.

==>Bonyeza Hapa Kuyasoma Majina Hayo

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA