Alichokizungumza Tundu Lissu Baada ya Kupata Dhamana ya Kutoka Mahabusu Jana


June 30 2016 Mbunge wa Singida Mashariki, ‘CHADEMA’ Tundu Lissu amesomewa shitaka lake la kutoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu June 28 2016 kinyume cha kifungu namba 32 ya sheria ya magazeti. Lissu amekana shtaka hilo na ameachiwa kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.

Inadaiwa Lissu alitoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya Kisutu kwa kumuita Rais ‘dikteta uchwara’, mtuhumiwa amedhaminiwa na wadhamini wawili na kesi imeahirishwa mpaka August 02 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa. Nje ya mahakama ya Kisutu, Lissu ameyazungumza haya……….

’Mimi nilidhani kwamba baada ya kauli yangu wenye busara wangenyamaza kimya lakini inaelekea busara inaonekana ni bidhaa adimu wameyaleta mahakamani, mimi na jopo langu la mawakili tutapata fursa ya kumuita huyo niliyemuita dikteta ‘uchwara’ kuja mahakamani kuiambia mahakama kuwa yeye si dikteta uchwara‘



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA