Mwanamume 'Adandia' Helikopta Kenya

Mwanamume mmoja katika mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya ameshangaza wengi baada ya kudandia helikopta ambayo imepaa na kuondoka naye.

Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara mashuhuri Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema.
Video zinazosambaa mtandaoni zinaonesha helikopta hiyo ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia kwenye vyuma vya helikopta hiyo.

Taarifa zinasema baadaye ndege imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo akapelekwa hospitalini.

Wengi wameeleza kushangazwa kwao na wengine wanalifanyia mzaha.
Baadhi wanasema mwanamume huyo alisahau leo ilikuwa Ijumaa tarehe 13, ambayo kwa baadhi ni siku yenye kutokea mabaya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA