Lady Jaydee Kumuanika Mpenzi wake Ambae ni Mrithi wa Gardner Leo!
Exclusive! Lejendari wa Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka kumi na tano,
Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee au Jide’, anatarajia kumuanika mrithi
wa aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa Kituo cha Radio CloudsFM, Gardner G.
Habash ndani ya saa 24, Ijumaa lina data kamili.
HABARI ZA KUAMINIKA
Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizothibitishwa na uongozi wa staa
huyo, Jide atamtambulisha mchumba wake huyo kwa mara ya kwanza ndani ya
Ukumbi wa Mlimani City leo, Dar ambapo pia atafanya shoo ya saa tatu
mfululizo, inayokwenda kwa jina la Naamka Tena.
“Itakuwa ‘sapraizi’ kwa mashabiki wote wa Jide ambapo sapraizi hii
itaendana na shoo ya kihistoria ya Naamka Tena atakayoipiga kwa saa tatu
akiwa na bendi yake (Lady Jaydee and The Band),” alisema mmoja wa
viongozi wanaomsimamia ambaye hakutaka kutajwa gazetini.
JIDE ALIPOTOKEA
Jide alifunga ndoa na Gardner Mei 14, 2005 ambapo waliishi na kufanikiwa
kuwa na mali mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba, Ukumbi wa Nyumbani
Lounge na Bendi ya Machozi
FIGISUGISU NA GARDNER
Mvutano wa wawili hao ulidaiwa kuanzia kwa Jide aliyeamua kuomba talaka
kwa kile kilichosemekana kuwa Gardner alipata kazi ya kutangaza redio
moja nchini Kenya hivyo kama angeenda huko wakati ni meneja wake,
angeshindwa kuwa naye huku pia figisufigisu nyingine nyingi zikijitokeza
kama kubadilisha jina la Ukumbi wa Nyumbani Lounge na kuwa M.O.G na
mambo mengine ikiwepo kusalitiana na kupigana.
WAFIKISHANA MAHAKAMANI
Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya
kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar, miezi
michache iliyopita na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo
na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka.
Maoni
Chapisha Maoni