Ommy Dimpoz akijibu kuhusiana na picha zilizo enea akiwa na Ex wa Diamond Platnumz 'Wema Sepetu' kitandani
Miongoni mwa stori zilizochukua headline mitandaoni hata kwenye magazeti
ni kuhusu picha ya hitmaker wa ‘Ndangushima’ Ommy Dimpoz akiwa na ex wa
Diamond Platnumz ,Wema Sepetu kitandani wamelala pamoja na picha
zingine zilizozua mjadala mkubwa.
Ommy Dimpoz amefanya mahojiano na mtangazaji wa Radio Clouds FM kwenye
kipindi cha Amplify ambapo mahojiano yake na mtangazaji huyo 'Millard
Ayo' yalikuwa kama ifuatavyo."Ni picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida, sasa nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori kwasababu mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori
May be nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha tuko chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli na tulikuwa tunakaa kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye mitandao unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye matembezi binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo tulienda South Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya utani utani nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza ninawambia wamuuliza aliyepiga picha hizo," Alisema Dimpoz.
Millardayo ; “…Wengi wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”
Ommy Dimpoz ; “…Sidhani kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu nimefahamia nao siku nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti kabla hawajakuwa kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi nianze kuelezea sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia siku nyingi kwa hiyo hata kama alikuwa katika uhusiano na Diamond yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa hivi hayawezi kunifanya mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu vyao personal…"Alisema.
Maoni
Chapisha Maoni