BARCELONA FC WANAKUJA BONGO NA WATACHEZA TAREHE 28/3/2015 UWANJA WA TAIFA NA NYOTA WATANZANIA SOMA HAPA
Mshambuliaji
wa zamani wa FC Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert
alizungumzia ujio wa magwiji FC Barcelona nchini mwezi wa tatu mbele ya
waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Sports Lounge uliopo jijini Dar
Es Salaam ,Pembeni ya Kluivert ni mwenyekiti wa DRFA Ndugu Almas
Kasongo. Magwiji hao wa Barcelona wanataraji kucheza na wachezaji nyota
wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa mnamo mwezi wa machi tarehe 28.
Mwenyekiti
wa chama cha soka mkoa wa Dar Es Salaam,Almasi Kasongo akizungumza
kwenye mkutano huo katikati na mwakilishi wa FC Barcelona pamoja na
Mwakilishi wa kampuni ya Prime Time Promotions Stuart Kambona ambao ni
waratibu wa mchezo huo.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema leo asubuhi
Timu
ya wachezaji nyota wa zamani wa Barcelona FC watacheza na wachezaji wa
zamani wa Tanzania, Tanzania All Stars Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa
jijini.Mwakilishi wa wachezaji wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert
alisema jana kuwa mechi hiyo itawahusisha wachezaji nyota wa Barcelona
wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta, Ludovic Giuly, Francesco Coco na
wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka tofauti.Kluivert alisema
kuwa kikosi chao kina wachezaji nyota ambao ni maarufu duniani na
wanaamini mechi itakuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa.
Alisema
kuwa yeye ni mwenyeji sana hapa Tanzania kwani huu ni ujio wake wa tatu
na anaamini kuwa jinsi mashabiki wanapenda sana mpira wa miguu, itakuwa
fursa kubwa kwao kuona vipaji vya zamani
ambavyo vimetukuka.“Ninafurahi kuja nchini Tanzania kwa mara ya tatu,
ni faraja kubwa pia kucheza hapa nchini kwa mara ya kwanza, naomba
mashabiki wa soka wajae uwanjani kuona mpira wenye ushindani,” alisema
Kluivert.
Mwakilishi
wa kampuni ya Prime Time Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu
hiyo ya Barcelona, Stuart Kambona alisema kuwa madhumuni ya mchezo huo
ni kudumisha mahusiano ya kibiashara ya mpira wa miguu baina ya Tanzania
na Hispania, kutangaza utalii na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya
nchi hizo mbili.
Kambona
alisema kuwa pamoja na kucheza soka siku hiyo, ujio wao pia utaitangaza
nchi nje ya mipaka yake na kuleta fursa nyingi hapa nchini.“Wachezaji
wa Barcelona wanataingia nchini siku mbili kabla ya mechi na watakuwa
zaidi ya 20, majina ya wachezaji wengine yatatangazwa baadaye, ila
tunaomba wadhamini wajitokeze kufanikisha na kufaidika na mechi hiyo,”
alisema Kambona.
Mwenyekiti
wa Chama cha soka cha mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almasi Kasongo
aliwaomba mashabiki wa soka kujiandaa kuangalia mechi hiyo kwa kufika
uwanjani.
Kasongo
alisema kuwa DRFA imefarijika sana kwa ziara hiyo na kuiomba Prime Time
Promotion kuhakikisha kuwa inapanua wigo kwa kuandaa mechi nyingi
ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo ya soka nchini.
Maoni
Chapisha Maoni