Polisi Marekani Yamkamata Mshukiwa wa Shambulio


Mtu aliyekuwa akitafutwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu katika miji ya New York na New Jersey amekamatwa baada ya kushambuliana na polisi kwa risasi.

Ahmed Khan Rahami, mwenye umri wa miaka 28 ni raia wa Marekani mwenye asili ya Afghan.
Alijeruhiwa katika mapambano hayo yaliyosababishwa kukamatwa kwake karibu na nyumba yake kwenye mji wa New Jersey.

Katika operesheni ya kumkamata mtuhumiwa huyo polisi wawili pia walijeruhiwa.
Meya wa mji wa New York, Bill de Blasio amesema kuna kila sababu kuamini kwamba shambulio hilo lilikuwa ni ugaidi.

Kwa upande wake Rais Barack Obama amewataka watu kuwa watulivu na kuongeza kuwa kila mtu ana mchango katika kuondoa hali hiyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA