CUF Waitupia Lawama Serikali kwa Kushindwa Kuwajibika na Kuruhusu Uingizwaji wa Simu FEKI
Jumuiya ya Vijana CUF (JUVICUF) imeitaka Serikali kubeba mzigo wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizwaji wa simu feki nchini. Kauli ya jumuiya hiyo imekuja wakati imebaki mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuzima simu feki zote. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa JUVICUF, Mahamoud Mahinda Ally alisema Serikali ilishindwa kutimiza wajibu wake wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini, hivyo inapaswa kuwajibika. Ally alisema Serikali ilipaswa kuziba mianya hiyo tangu mwanzo na kwamba inachofanya sasa ni kukosa huruma kwa watu wake. Alisema kitendo cha wananchi kuachwa wakinunua simu feki siku za nyuma bila ya kudhibiti uingizwaji wake nchini ni kutozingatia matakwa ya haki za binadamu. “Kuruhusu simu feki ziingie nchini, kisha kuzizima ni mapambano ambayo Serikali inapambana dhidi ya wananchi wake,” alisema Ally. Akizungumzia kuhusu hilo, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocen...