AFISA TARAFA WA KIBITI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushongi akizungumza na waandishi wa habari kuhusina na tukio la kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Afisa Tarafa wa Kibiti kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Kitunda.(Picha na Victor Masangu) NA VICTOR MASANGU, PWANI JESHI la polisi Mkoa wa Pwani limemkamata na kumfikisha mahakamani Afisa Tarafa wa Kibiti Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Selemani Mpangile almaarufu babu konyeza kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi kitunda. Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushogi amesema kwamba tukio hili limetokea juzi majira ya saa 10 jioni ambapo mtuhumiwa aliamua kutenda kosa hilo kinyume na sheria na taratibu za nchi. ...