Simulizi ya mwanamke mmoja ambaye anadai kuwa ndoa yake iliingia doa siku ya harusi
Harusi huwa ni jambo la kheri ambapo sherehe hiyo huwa inawavutia wengi duniani kote ingawa baadhi ya wanawake katika maeneo kadhaa ya dunia, sherehe hiyo hugeuka kuwa janga ambalo wanashindwa kulisahau kutokana na sababu tofauti tofauti.
Katika mataifa ya kiarabu na kiislamu, wanawake huwa wanatarajiwa kuwa mabikiwa wakati wanapoolewa.
Idhaa ya kiarabu ya BBC ilizungumza na baadhi ya wanawake kuhusu uzuri wa usiku wa harusi katika kujenga ndoa zao na namna gani ukosefu wa elimu ya ngono unavyoathiri ndoa zao.
Somayya aliingia kwenye mvutano na familia yake mara baada ya familia yake kumkatalia kuolewa na mwanaume aliyempenda kwa dhati, Ibrahim.
Hakutegemea hata kidogo kuwa maisha yake yangeweza kubadilika na ndoto zake kupotea.
Ilikuwa ni siku ya kwanza kukutana na mume wake inayofahamika kama "night of entry" kipindi ambacho mapenzi yote yaliisha kutokana na kutolewa kwa ubikira wake.
Somayya, mwenye umri wa miaka 23, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Damascus huko nchini Syria alikuwa anakaribia kumaliza shahada yake ya lugha ya kiarabu.
Wakati huo huo alikuwa ana mahusiano na Ibrahim, ambaye waliweka nadhiri kuwa pamoja kipindi atakapomaliza masomo yake ya elimu ya juu.
Licha ya kwamba familia yake ilipinga ndoa yao lakini waliendelea na kufunga ndoa.
Binti huyo aliolewa na Ibrahim huku wakiwa na mapenzi ya dhati.
Somayya aliwaambia familia yake yote kuwa ana furaha sana kuwa na Ibrahim.
Lakini siku ya usiku wa harusi yake mambo yakawa ndivyo sivyo, alipata mshtuko baada ya kukutana kimwili na mume wake.
"Nilionyesha ushirikiano lakini sikuweza," Somayya alisema.
'Mahaba yalipotea mara baada ya kukutana'
Mahaba ambayo nilikuwa nayo yalipotea ghafla.
Uso wake ulibadilika rangi na muonekano , alieleza kuwa alijua kuwa anadhani yeye sio bikira mara alipodai kuwa "mbona hakuna damu yeyote kwenye shuka".
Wanawake wengi hutoka damu kuashiria kuwa wametoa ubikira wao lakini madaktari na wataalamu wa afya wanasema kuwa sio lazima kwa wanawake kutoka damu siku anapovunja ubikira wake.
Kuna sababu nyingi ambazo hupelekea damu kutotoka siku mwanamke anapokutana na mwanaume kwa mara ya kwanza, kuna wanawake ambao wamezaliwa hivyo yaani asili yao huku wengine labda alitoa ubikira wake kwa bahati mbaya akiwa mtoto, labda aliumia.
Somayya anasema kuwa jinsi mume wake alivyohamaki na kushindwa kumuelewa kuwa alikuwa bikira, jambo hilo linamuumiza moyoni bila yeye kutambua.
"Hakujaribu hata kuongea na mimi kuniuliza ilikuaje, nilihisi kutengwa na sawa na mthumiwa anayesubiri hukumu. Kabla ya ndoa yetu tuliongea mambo mengi sana na tulizungumzia kuhusu usiku wetu wa harusi kuwa wa kipekee katika maisha yetu lakini hali ilibadilika".
"Tulihisi tulijuana sana lakini ishara ya kutokuwa bikira ilitufanya kuwa kama watu wasiojuana."
Licha ya kwamba tukio kama la Somayya sio geni katika jamii inayomzunguka lakini hakuwahi kukutana nalo yeye mwenyewe.
Vilevile alidhani tu kizazi cha sasa maono yao ni tofauti na enzi za mababu zetu kutokana na kupata elimu ya kutosha.
Somayya aliamua kwenda kwa mtaalamu wa afya ya uzazi ili kubaini tatizo lake na kuambiwa kuwa alizaliwa hivyo.
Mume wake alipata aueni na kuanza kuonyesha tabasamu katika uso wake lakini muda ulikuwa umepta tayari.
Somayya alikuwa alikuwa ameshaamua kutaka talaka haraka iwezekanavyo.
Alieleza kuwa alieleza kuwa maamuzi yake ya kutaka talaka yalikuja mara baada ya mume wake alipoanza kuwa kama mtu asiyemfahamu kabisa.
Nilikuwa sijui nini anawaza na maamuzi gani atachukua na sikujiona kuwa salama hata kidogo.
Tangu wakati huo Somayya alipata matatzo ya kisaikolojia. Hakutaka wageni na hakutaka hata kutoka nje.
Kwa kipindi cha miezi mitatu alikutana na mume wake kimwili bila ridhaa yake. " Sikumtaka tena na sikuhisi chochote kabisa kwa sababu mapenzi yangu yaliisha usiku wa harusi yetu" alisema.
Mtaalamu anasema kuwa kisa kilichomkuta Somayya sio kipya katika jamii yake , kwa sababu kuna wengi ambao huwa wanajifungia ndani ili kujizuia kushangaliwa na kuhukumiwa na jamii.
Lakini baadae watoto wanaathirika kwa kushindwa kupata ufahamu wa masuala haya kwa uhuru na mara kwa mara.
BBC iliwahoji wanaume 20 namna walivyojisikia walikutana na wapenzi wao kwa mara ya kwanza bila kuona ishara ya kuwa bikira.
Wanaume wenye kati ya umri wa miaka 20 na 45, waliooa na wasiooa lakini wakiwa na taaluma mbalimbali kama madaktari, walimu na wengine ambao wana uelewa lakini majibu yao mengi yalionekana kuwa hasi.
Wengi wanaamini kuwa doa la damu katika shuka ndio uthibitisho wa mwanzo mzuri wa maisha ya ndoa yenye furaha na uelewano.
Miezi michache baadae Somayya alimwambia mume wake kuhusu nia yake ya kutaka waachane na hawezi kubadili mawazo yake kwa sababu alimuogopa na hakuwa na mapenzi naye tena mara baada ya kukutana mara ya kwanza.
Alimwambia pia jinsi alivyoshangazwa na jinsi alivyopokea hali yake kwa kutomjali kabisa na kuanza kumshusha viwango.
Mume wake alishangazwa na maamuzi hayo na kuhisi alikosea kutomuuliza kama aliwahi kulala na mwanaume mwingine kabla yake au la.
Mume wake alimwambia kuwa hawezi kumuacha au kutoa talaka wakati yu hai na kumshauri kufikiria tena kwaumakini kuhusu uamuzi aliochukua asije kujutia.
"Jamii yetu haina usawa", Somayya alisema, "wanaume ni sawa kujihusisha na mahusiano kabla ya ndoa lakini sio wanawake, mwanamke anapojihusisha na mapenzi kabla ya kuolewa anaweza kukataliwa katika jamii na hata kuuwawa."
Ni jambo la aibu kwa wanawake huku kwa wanaume ni kitu cha kawaida.
Maoni
Chapisha Maoni