Bosi wa McDonald Steve Easterbrook afukuzwa kazi kisa uhusiano wa kimapenzi.
McDonalds imemfuta kazi kiongozi wa juu baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi.
Kampuni hii kubwa ya chakula imesema kuwa uhusiano huo ulikua wa makubaliano baina yao lakini umekiuka sera za kampuni na kuonesha maamuzi mabaya.
katika barua pepe iliyotumwa kwa wafanyakazi, mfanyabiashara huyo muingereza alikiri kuwa na uhusiano na kusema kuwa alifanya makosa.
''kwa kufuata taratibu za kampuni nakubali ni muda sasa wa mimi kuondoka'' alisema Bosi huyo.
Bwana asterbrook, mwenye umri wa miaka 52, ambaye ameachana na mkewe, amefanya kazi katika kampuni ya McDonalds tangu mwaka 1993, kama meneja huko London kabla ya kuteuliwa katika wadhifa huo.
Aliondoka mwaka 2011 na kuwa bosi wa Pizza Express na baadae kwenda katika kampuni ya chakula ya Asia kisha kurudi McDonalds mwaka 2013, mwaka 2015 alichagulia kuwa mwenyekiti mtendaji wa McDonald's .
Unaweza pia kusoma:
Wakati wa uongozi wake, McDonald's iliongeza usambazaji wake pamoja na malipo kwa njia ya simu ili kuharakisha zaidi utendaji kazi.
Alijiuzulu kama kiongozi wa kampuni hiyo na kujiondoa katika nyadhifa zote kwenye bodi ya wakurugenzi.
Sera na sheria za kampuni zinapiga marufuku mahusiano ya kimapenzi baina ya wafanyakazi na viongozi wao.
McDonald's imekua ikikosolewa kwa jinsi inavyowalipa wafanyakazi wake kipato kidogo, kwa upande wa kiongozi wake Easterbrook mwaka jana alikumbwa na kashfa ya kulipwa pesa nyingi zaidi, mshahara wake ulikua mara 2,214 ya mshahara wa mfanyakazi wa kawaida.
Nafasi ya bwana Easterbrook itachukuliwa na Chris Kempczinski ambaye kwasasa ni rais wa McDonald's ya Marekani. Kempczinski alisema kuwa anamshukuru sana bwana Easterbrook kwa kumpeleka McDonalds.
''Steve amenileta McDonalds, na alikua mshauri wangu na muvumilivu sana''
Maoni
Chapisha Maoni