Ndege ya C-130: Mabaki yake yapatikana yakiolea katika maji Chile
Haki miliki ya picha Image caption Mabaki ya ndege yalipatikana yakiolea katika eneo ambalo ndege hiyo ilitoweka siku ya Jumatatu. Maafisa wa Chile wanasema kwamba wamezuia mabaki yanayoaminika kutoka katika ndege ya kijeshi iliotoweka siku ya Jumatatu. Wanasema kwamba mabaki hayo yalipatikana yakiolea kilomita 30 kutoka eneo ambalo ndege ya wanahewa wa Chile aina ya C-130 Hercules inayobeba mizigo ilikuwa na mawasiliano ya mwisho. Vifusi hivyo vilipatikana katika maji yanayojulikana kama mkondo wa Drake. Wengi wahofiwa kufariki baada ya ndege kuangukia nyumba DR Congo Hili ndilo taifa hatari zaidi kusafiri kwa ndege? Siri yafichuliwa kuhusu mfumo wa oksijeni wa Boeing 787 Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji wa kusini wa Chile wa Punta Arenas ikielekea katika kambi ya kijeshi ya Antarctica ambapo rais wa taifa hilo Eduardo Frei Montalva alikuwa. Vifusi hivyo huenda vinatoka kutoka tangi la mafuta la ndege hiyo , kulingana na kamanda wa jeshi la wanahewa Eduardo Mosqueira ...