TRUMP AKIRI KWAMBA ANACHUNGUZWA MAREKANI
Trump akiri kwamba anachunguzwa Marekani
16 Juni 2017
Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya
Sambaza habari hii Facebook
Sambaza habari hii Twitter
Sambaza habari hii Messenger
Sambaza habari hii Email
Mshirikishe mwenzako
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Donald Trump amekana tuhuma kwamba maafisa wake walishirikiana na maafisa wa Urusi
Rais wa Marekani Trump amethibitisha kwamba anachunguzwa yeye binafsi kutokana na hatua yake ya kumfuta kazi mkuu wa Shirika la Uchunguzi wa Jinai la Marekani FBI James Comey.
Kupitia Twitter, Bw Trump amekariri kwamba uchunguzi unaoongozwa na mwendesha mashtaka maalum kuhusu tuhuma kwamba maafisa wa Urusi waliingilia uchaguzi wa mwaka 2016 ili kumfaa Trump hauna msingi.
Ni mara ya kwanza kwa Bw Trump kuzungumzia taarifa kwenye magazeti kwamba anachunguzwa kwa tuhuma za kuhujumu mifumo ya haki kwa kumfuta kazi Bw Comey.
Waziri mkuu Australia amkejeli rais wa marekani Donald Trump
Sessions: Sikufanya mikutano ya siri na maafisa wa Urusi
Trump aisifu Saudi Arabia kwa kuitenga Qatar
Awali, taarifa kwenye vyombo vya habari Marekani vilikuwa vimeripoti kwamba wasaidizi wake pamoja na watu waliojitolea kusaidia katika kundi lake la mpito wameamrishwa kuhifadhi nyaraka zote kuhusiana na uchunguzi huo wa madai kuhusu Urusi.
Taarifa zinasema mawakili wa maafisa hao wa Trump wametakiwa kuhifadhi nyaraka zote zinazohusiana na Urusi, Ukraine na washauri wengine kadha wa kampeni.
Kuna makundi kadha yanayofanya uchunguzi, kundi moja likiongozwa na mkurugenzi wa zamani wa FBI Robert Mueller, ambayo yanachunguza iwapo maafisa wa Trump walishirikiana na maafisa wa Urusi wakati wa kampeni.
Bw Trump amekana tuhuma hizo.
Maoni
Chapisha Maoni