CRISTIANO RONALDO MMMH!

Cristiano Ronaldo 'anataka kuihama' Real Madrid juu ya kodi 16 Juni 2017 Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Email Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Cristiano Ronaldo amekuwa Real Madrid kwa miaka minane Nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amekereka sana baada ya tuhumiwa kwamba alifanya ulaghai wakati wa ulipaji ushuru na anataka kuihama klabu hiyo, duru zimeiambia BBC. Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanamtuhumu Ronaldo, 32, kwa kutumia ulaghari kutolipa mamilioni ya ushuru. Amekanusha tuhuma hizo. "Anahisi kwamba amekuwa mkweli, ana sifa nzuri na alifanya kila kitu ipasavyo," ameongeza mdokezi. Mkataba wa Ronaldo katika klabu hiyo ya Madrid una kifungu cha euro bilioni moja (£874.88m), ambacho kinafaa kufikishwa ndipo afunguliwe kutoka kwa mkataba wake. Mdokezi aliongeza: "Amehuzunika sana na ameudhika kwa kweli." kumfungua kutoka kwa mkataba huo wake. _96516050_gettyimages-676397152 "Hataki kukaa tena Uhispania. Kwa sasa, anataka kuondoka." Cristiano Ronaldo hakulipa kodi Ronaldo ashinda tuzo ya FIFA Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa £80m, alitia saini mkataba wa miaka mitano katika klabu hiyo Novemba mwaka 2016. Mreno huyo anaweza kwenda China, lakini washauri wake wangependa aendelee kucheza soka Ulaya, pengine ahamie Paris St-Germain ya Ufaransa au arejee Ligi ya Premia. Ronaldo, aliyewasaidia Real kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhumiwa kulaghai maafisa wa serikali ushuru wa takriban euro 14.7m (£13m; $16m) kati ya 2011 na 2014. Haki miliki ya picha Getty Images Real Madrid wametoa taarifa wakisema wana imani kamili na mchezaji wao huyo, na kwamba wana uhakika atathibitisha kwamba hana makosa. Sanamu ya kushangaza ya Ronaldo Cristiano Ronaldo aandika historia kufikia magoli 100 Wasanii na wachezaji matajiri zaidi duniani watajwa Msimu wa 2016-17, Ronaldo alisaidia Real kushinda taji la ligi Uhispania wka mara ya kwanza tangu 2012, na pia kutetea taji lao la Kombe la Klabu Bingwa Ulaya. Ronaldo, aliyeshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya pia akiwa na Manchester United mwaka 2008, amefunga mabao 105 katika michuano hiyo, 11 zaidi ya mpinzani wake wa Barcelona Lionel Messi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA