Utajiri wa Diamond Umefikia Shilingi Bilioni 8.6


Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.

Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA