Mama yake Halima Mdee alia na serikali ya Magufuli



Mama mzazi wa Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mama Theresia Mdee ameilalamikia Serikali ya Awamu Ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kutokana na yanayomsibu mwanae.
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya Jeshi la Polisi kupekuwa nyumba ya Halima Mdee, ambaye wiki hizi mbili zilikuwa chungu kwake baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi na kulazwa rumande.
Mama huyo alieleza kuwa kinachofanywa na serikali dhidi ya mwanae ni uonevu wa dhahiri na kumnyima haki.
“Hii serikali kwakweli tunaona kwamba haitutendei haki. Hayo yote wanayomfanyia huyu mtoto hakuyafanya. Wanamuweka ndani bila sababu, wanakuja kumsachi hakuna kitu… ni kiasi cha kumuumiza tu na kumkandamiza ili asiweze kufanya kitu,” alisema.
Hata hivyo, Mama huyo alitahadhalisha kwamba vitendo hivyo vinavyofanywa dhidi ya mwanae huenda vikawa chanzo cha kumkuza zaidi, “Sasa wajue kwamba wanamtia moshi”.
Mdee alishikiliwa na polisi kufuatia vurugu zilizoibuka katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, baada ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kutangaza kuahirisha uchaguzi. Uliokuwa umepangwa kufanyika siku hiyo (Jumamosi, Februari 27).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nani aligharamia ukarabati wa kifahari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa

Abu Bakr al-Baghdadi: Nguo ya ndani ya kiongozi wa IS 'iliibiwa' kufanya uchunguzi wa DNA