Hiki ndicho kilichofikiwa katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu Kahama.
.tz/media/image/kaha.jpg" />
Kesi
ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi
mwaka jana iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya
CHADEMA jimbo la Kahama mjini Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea wa CCM
Mh.Jumanne Kishimba imeendelea leo katika mahakama ya wilaya ya Kahama.
Kesi hiyo amnbayo iliendelea kuunguruma leo majira ya saa tano
kamili huku wananchi waliofika mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa
kesi hiyo wakiilalamikia mahakama kutoweka vipaza sauti hali
inayosababisha idadi kubwa ya wananchi waliofika kusikiliza kesi hiyo
kushindwa kuelewa nini kinaendelea.
Aidha baada ya jaji Moses Mzuna kusikiliza hoja za kila upande na
kuridhika na maelezo aliagiza pande zote mbili kuleta mashahidi wao ili
waanze kutoa ushahidi na kuahirisha kesi hadi kesho siku ya jumatano
tar.02/03 ambapo kesi itaendelea.
Maoni
Chapisha Maoni