LADY JAY DEE AJIBU TETESI ZA KURUDIANA NA GARDNER G HABASH
Msanii
mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Lady Jaydee amefunguka kuhusiana
na tetesi kwamba amerudiana na aliyekuwa mume wake Gadner G Habash.
Aliulizwa
swali hilo na mtangazaji Sam Misago katika kipindi cha E News
kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.
“Watu
wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote,
sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania wanipende kama
mimi kama Jaydee na si vinginevyo,”alisema Jaydee.
Msanii huyo ameibuka tena na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndindindi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.
Maoni
Chapisha Maoni